Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dereva City Boy kortini

Muktasari:

Awali, Hakimu wa Mahakama hiyo,  Joyce Minde alimweleza mshtakiwa kuwa atasomewa makosa yake yote lakini hataruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikilza kesi za mauaji.

Singida. Dereva wa basi la City Boys, Jeremia Sempungwe (33) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida akikabiliwa na  makosa 30 ya kusababisha vifo vya abiria 30 bila kukusudia.

Awali, Hakimu wa Mahakama hiyo,  Joyce Minde alimweleza mshtakiwa kuwa atasomewa makosa yake yote lakini hataruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikilza kesi za mauaji.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali mkoani Singida, Zakaria Ndaskoi alidai kuwa Julai 2, mwaka huu Sempungwe akiendesha basi kutokea Dar es Salaam kuelekea Kahama, basi hilo liligongana uso kwa uso na basi lingine la kampuni ya City Boys na kusababisha vifo vya abiria 30 bila kukusudia na majeruhi 54.