Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo Vodacom, wenzake wakiri makosa

Vigogo wa kampuni ya Vodacom wakiwakatika mahakamaya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dares Salaam wakikabiliwa na mashtaka ya kuhujumu Uchumi . Picha na Said Khamis

Muktasari:

  • Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom Hisham Hendi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 10, likiwamo la kuongoza genge la uhalifu na kuisababishia hasara Serikali ya Sh5, 892,513,000.

Dar es Salaam.  Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, Hisham Hendi na wenzake wanane wamekiri mashtaka yao.

Hendi na wenzake wamekiri mashtaka yao leo Alhamisi Aprili 11, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hendi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka wanakabiliwa na mashtaka 10, likiwamo la kuongoza genge la uhalifu na kuisababishia hasara Serikali ya Sh5, 892,513,000.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Simon alidai kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amewasilisha hati ya kuruhusu mahakama ya Kisutu kusikiliza shauri hilo.

Simon baada ya kuwasilisha hati ya DPP ameomba kuwasomea mashtaka yao na baada ya kuwasomea mashtaka yao, washtakiwa hao wamekiri.

Washtakiwa baada ya kukiri mashtaka hao,  upande wa mashtaka kwa sasa wameanza kusomewa maelezo ya awali (PH), mmoja baada ya mwingine.

Mbali na Hendi, washtakiwa wengine ni Ahmed Ngassa ambaye ni meneja uendeshaji wa biashara kutoka kampuni ya Inventure Mobile Tanzania Ltd/ A Tala Tanzania; mtalaamu wa Tehama na raia wa Kenya, Brian Lusiliola; na kampuni ya Inventure Mobile Tanzania Ltd iliyopo katika jengo la Tanzanite Park, eneo la Victoria.

Washtakiwa wengine ni Mkuu wa Idara ya Mapato wa Kampuni ya Vodacom, Joseph Nderitu; Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Vodacom, Olaf Mumburi;  Mkuu wa Idara ya Mauzo wa Vodacom, Joseph Muhere.

Wengine ni Meneja wa Fedha wa Vodacom, Ibrahim Bonzo na Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom.

Kesi inaendelea