Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge ataka mihimili ya dola iogopane

Mbunge wa Jimbo la Mwanga, Joseph Tadayo akichangia mchango katika Mapendekezo ya Mpango wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 bungeni jijini Dodoma.

Muktasari:

  • Wabunge wameendelea kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2025/26 na Mwongozo wa Mapendekezo ya bajeti kwa mwaka 2025/26, huku hoja ya mihimili ya dola yaani Bunge, Serikali na Mahakama iogopane.

Dodoma. Suala la matumizi mazuri ya Serikali limeendelea kupigiwa kelele na wabunge huku Mbunge wa Mwanga (CCM), Joseph Tadayo akitaka mihimili mitatu ya dola kukaa kwenye mazingira ya kuogopana isiwe na urafiki wa kupitiliza.

Wabunge wameyasema hayo leo Jumatano, Novemba 6, 2024 wakati wakijadiliana na kushauri kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2025/26 na Mwongozo wa Mapendekezo ya bajeti kwa mwaka 2025/26.

Akichangia mjadala huo, Tadayo amesema Katiba ya Tanzania ni nzuri na endapo itatumiwa vizuri hakuna anguko litakalotokea katika utawala bora.

Hata hivyo, ametaka mihimili ikae kwenye mazingira ya kuogopana kidogo isiwe na urafiki wa kupitiliza.

“Tunatakiwa tufike mahali mwekezaji akitaka kuja kuwekeza Tanzania asijiulize anamfahamu nani au waziri gani, aje kwa sababu anafahamu mifumo yetu iko imara na impatie kila anachokitaka,” amesema.

Tadayo amesema Katiba ya Tanzania ina uwezo wa kutoa vitu vyote lakini kinachopungua ni utashi wa watu.

Amesema utashi huo ni kuipenda, kujifunza Katiba, kuikimbilia na kuheshimu.

Tadayo amesema kuitumia Katiba hiyo ni kama unafanya jambo lako uifuate kama mkuki na kama kuna mtu anakuingilia haki yako uitumie kama ngao.

“Tunaweza kuwa na Katiba nzuri lakini kama hakuna utashi wa kuitumia itabaki kama kiapo bila kutufaa chochote,” amesema.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jenejelly Ntate ameshauri kuundwa kwa kamati ya matumizi itakayoangalia matumizi ya Serikali.

“Kitu kimoja kinafanywa na wizara zaidi ya tatu. Nishawahi kuchangia katika Bunge hili kuwa kilimo wanachimba mabwawa ya umwagiliaji yaleyale wanayochimba yanaweza kuvutwa kwa wananchi,” amesema.

Amesema kwa kufanya kwa pamoja kunaweza kupunguza matumizi ya Serikali na kuishauri Tume ya Mipango kufanya kazi hiyo.

 Mbunge wa Mbalali (CCM), Bahati Ndingo amesema ongezeko la watu haliakisi kuimarika kwa uchumi wao  na kutaka Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji kuonyesha ni namna gani ongezeko hilo linaakisi uchumi wa Tanzania.

“Kwa sababu hali iliyopo sio nzuri kama watu 100, watu 87 ni tegemezi ni lazima mpango uonyeshe ni namna gani ongezeko letu kama Taifa la watu linaakisi ongezeko la uchumi,” amesema Bahati.

Mbunge wa Kinondoni (CCM), Abbas Tarimba ametaka Serikali kwenda bungeni na mipango ambayo itaongeza uwezo wa ukusanyaji wa kodi.

Ametaka pia Serikali ipeleke bungeni mfumo wa ukaguzi wa kodi kila mwaka. “Tujifunze  kwenye nchi zilizofanya vizuri katika Kodi ya Ongezo la Thamani (VAT).

Amesema tangu kuanzishwa mashine ya EFDs mwaka 2010, Serikali imekuwa ikitoa elimu tu ambayo haijaleta matokeo makubwa.

“Si rahisi mtu kulipa kodi anavyopenda kwa sababu unachukua hela yake hivyo tungekuwa na mifumo ya kidijitali kwa waliofanya vizuri katika VAT. Tuwe na mifumo inayomlazimisha mtu kutoa risiti ya kidijitali tuondokane na mtu hadi uombe,”amesema.

Mbunge wa Ole (CCM), Juma Hamad Omar amesema kuwa reli ya kisasa ya SGR, inasafirisha abiria na haisafirishi mizigo. “Ili ipate faida ni lazima ijikite kwenye kusafirisha mizigo.

Amesema kwa wao waliotembea katika nchi mbalimbali wamejionea reli ni ya Serikali kuna watu tofauti wana mabehewa kupitia usafiri wa reli hizo.

“Kwa hiyo unawapa nafasi sekta binafsi kushiriki katika usafirishaji ambao bila shaka hawatabeba  abiria shauku kubwa itakuwa ni kubeba mizigo na hivyo itaipunguzia mzigo Serikali,” amesema.

Amesema katika vipande vya reli vilivyobakia kujengwa kuna haja ya kwenda katika mpango wa Ushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi (PPP),