Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikoa minne kuanza uboreshaji daftari la mpigakura

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INCE), imeanza maandalizi ya mzunguko wa tisa kati ya 13 ya uboreshaji wa daftari hilo na mikoa ya Songwe, Njombe, Rukwa na Ruvuma itahusishwa

Songea. Baada ya kuanza katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Kigoma, hatimaye uboreshaji wa daftari la kudumu la mpigakura umefika wilayani Songea mkoani Ruvuma, huku wananchi wakionywa kuhusu kujiandikisha zaidi ya mara moja.

Kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kujiandikisha zaidi ya mara moja ni kosa la jinai na adhabu yake ni faini, kifungo au vyote kwa pamoja.

Hayo yameelezwa leo, Jumatano Januari 1, 2025 na Mkurugenzi wa Idara ya Daftari na Tehama wa INEC, Stanslaus Mwita alipozungumza na wadau mbalimbali kuhusu uboreshaji wa daftari hilo.

Amesema tume hiyo imeanza maandalizi ya mzunguko wa tisa kati ya 13 ya uboreshaji wa daftari hilo na mikoa ya Songwe, Njombe, Rukwa na Ruvuma itahusishwa.

Kwa mujibu wa Mwita, uboreshaji huo utafanyika kwa siku saba kuanzia Januari 12 hadi 18, 2025 na vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

Amesema mfumo uliopo sasa unamwezesha mpiga kura aliyepo kwenye daftari kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zake au kuhama kituo kwa kutumia aina yoyote ya simu ya kiganjani au kompyuta.

Akizungumzia masharti ya kifungu cha 168 cha sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani namba 1 ya mwaka 2024, Mwita amesema kadi za mpigakura zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 zenye jina la INEC ni halali na zitaendelea kutumika kwenye chaguzi zijazo.

Mdau wa uchaguzi huo, Victor Haule amewasisitiza wananchi kujitokeza kuboresha taarifa zao katika daftari hilo.

Uboreshaji wa daktari hilo, ulizinduliwa rasmi Julai 20, 2024 mkoani Kigoma mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Tayari mikoa 19, imekamilisha uboreshaji huo, huku Mbeya na Iringa ikitarajiwa kukamilisha kesho.