Ndesamburo, gwiji aliyetawala siasa Moshi
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro,Phillemon Ndesamburo akionesha tuzo aliyopewa na taasisi ya Mission to the World International enzi za uhai wake, ikiwa ni kutambua mchango wake katika jamii. Hafla hiyo ilifanyika mkoani Arusha hivi karibuni. Picha na Filbert Rweyemamu
Muktasari:
- Kwa wale ambao hawamjui, watajiuliza “Ndesamburo ni nani?”
- Ndesamburo, aliyezaliwa Februari 19, 1935, amefariki akiwa na umri wa miaka 82.
- Binafsi nilimfahamu Ndesamburo maarufu kama mzee Ndesa mwaka 1994, kulipofanyika uchaguzi wa Diwani wa Kiborlon uliokuwa na ushindani mkubwa kati ya CCM na Chadema.
Moshi. Ni kweli mbunge wa zamani wa Moshi Mjini na mwanasiasa mkongwe wa siasa za mageuzi nchini, Philemon Ndesamburo hatunaye.
Kwa wale ambao hawamjui, watajiuliza “Ndesamburo ni nani?”
Ndesamburo, aliyezaliwa Februari 19, 1935, amefariki akiwa na umri wa miaka 82.
Binafsi nilimfahamu Ndesamburo maarufu kama mzee Ndesa mwaka 1994, kulipofanyika uchaguzi wa Diwani wa Kiborlon uliokuwa na ushindani mkubwa kati ya CCM na Chadema.
Ndesamburo, ambaye ni mwasisi wa Chadema kama alivyo Edwin Mtei, alikuwa na matumaini ya kushinda uchaguzi huo, kabla ya ndoto hiyo kuvurugwa na Augustine Mrema, siku moja kabla ya uchaguzi.
Kulikuwa hakuna jinsi ya CCM kumshinda Ndesamburo, isipokuwa kumtumia Mrema ambaye wakati huo alikuwa Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Moshi Vijijini.
Ndesamburo, ambaye ni miongoni mwa waasisi wa mageuzi kuanzia miaka ya tisini akiwa na kadi namba 10 ya Chadema, hakukata tamaa.
Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 akajitosa tena. Safari hii aligombea ubunge wa Moshi Mjini, lakini akashindwa na mgombea wa NCCR-Mageuzi, Joseph Mtui wakati huo Mrema akiwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na nyota yake ilikuwa iking’aa.
Habari zaidi pata Mwananchi