Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Necta yataja sababu ya kutotangaza wanafunzi, shule bora

Muktasari:

  • Baraza la Mtihani la Taifa (NECTA), limetangaza sababu ya kutopanga na kutangaza shule na wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, likisema limebaini hakuna tija ya kufanya hivyo.


Dar es Salaam. Baraza la Mtihani la Taifa (NECTA), limetangaza sababu ya kutopanga na kutangaza shule na wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, likisema limebaini hakuna tija ya kufanya hivyo.

Kauli hiyo imetolewa leo, Januari 29, 2023 na Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Amasi wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne kwa wanafunzi wa 2022.

"Ina tija gani kumtaja mmoja kati ya shule nyingi na tena bahati mbaya unamlinganisha mtu na mwingine ambaye hawakusoma kwenye mazingira yanayofanana,” amesema.

Amefananisha kitendo cha kupanga orodha ya shule 10 bora zilizofaulisha zaidi ni sawa na kuzitangazia soko badala ya ushindani.

"Kutangaza shule ya kwanza huenda tunaifanyia biashara (marketing) , kwa hiyo jambo ambalo halina tija tumeona tuondokane nalo," ameeleza.

Awali, Necta ilianza utaratibu wa kutotaja 10 bora katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana kwa kile ilichokifafanua kuwa imeondokana na mazoea.