Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Serikali ikiwezeshe kilimo kuwa cha biashara’

Muktasari:

  • Pamoja na kuzalisha chakula kingi kuliko mahitaji ya Watanzania, imeelezwa upo uwezekano wa nchi kuzalisha zaidi na kuuza mazao nje ya nchi.

Dar es Salaam. Mwandishi Mkuu wa gazeti la Mwananchi Elias Msuya amesema licha ya Tanzania kuzalisha chakula kingi kuliko mahitaji, bado kuna uwezekano wa kuzalisha zaidi kwa ajili ya mahitaji ya ndani na kufanya biashara nje ya nchi.

Pia kuongezwa kwa uzalishaji kutaifanya nchi kuwa na mazao ya ziada ambayo inaweza kuuza nje na kuzalisha ajira.

Ameyasema hayo leo Agosti 30 wakati akizungumza katika mjadala wa Twitter space ulioandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) uliobebwa na mada isemayo nini kifanyike kuboresha kilimo biashara na uhifadhi wa chakula.

Msuya amesema jitihada za kuongeza uzalishaji zinaakisiwa na takwimu ambazo kwa sasa zinaonyesha kushuka.

"Uzalishaji wa mazao ya nafaka na yasiyo na nafaka umepungua kutoka tani zaidi ya 18.66 milioni mwaka 2020/21 hadi zaidi ya tani 17.4 milioni mwaka 2021/22. Mazao yasiyo ya nafaka ni pamoja na muhogo,m viazi na ndizi," amesema Msuya.

Amesema kilimo kinaweza kutumika kama bishara katika mazao kama pamba, pareto, kahawa na mazao ya chakula yanaweza kuwa fursa ya bishara kubwa.

"Ili kufanikisha hili Serikali ina jukumu la kuwekeza kwenye kilimo kwa kuwa ndiyo sekta inayoajiri watu wengi. Tumeona juhudi za kuongeza bajeti lakini bado haitoshi, tuko chini ya lengo la bajeti ya kilimo inatakiwa kuwa asilimia 10 ya bajeti kuu," amesema Msuya.

Amesema kama nchi inaweza kufanya uzalishaji hadi tani 50 kwa mwaka ili iweze kuuza na kuleta ajira kwa vijana na kukuza uchumi jambo ambalo pia litachochea ukuaji wa kilimo.

"Kwa sasa ukuaji wa kilimo umeshuka kutoka asilimia 4.9 mwaka 2020 hadi 3.9 mwaka 2021  lakini ukuaji unatakiwa walau kufikia asilimia 6," amesema Msuya.

Amesema mchango wa kilimo pia bado uko chini ya asilimia 30 na hii inaonyesha kuwa kilimo bado ni kitu cha kujikimu hakijawekewa nguvu kubwa.