Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Songea wachekelea uteuzi wa Dk Nchimbi ugombea mwenza CCM

Muktasari:

  • Wengi wakumbuka kazi zake alizozifanya alipokuwa mbunge wa Jimbo la Songea Mjini.

Songea. Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameonyesha furaha na kuridhishwa na uteuzi wa Balozi Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

Wamesema ni kiongozi makini, mzalendo, mchapakazi, asiyeweza kuyumbishwa na mfuatiliaji wa karibu wa masuala muhimu ya nchi.

Kwa msingi huo, wanaamini kuwa miradi ya maendeleo ya kimkakati itatekelezwa na kukamilika kwa wakati.

Jana, Chama cha Mapinduzi (CCM) kilipitisha jina la Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliyetangazwa rasmi kugombea kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.

Samia alimpendekeza Dk Nchimbi katika mkutano mkuu  jana Jumapili Januari 19,2024 na kuhitimishwa jana na itakumbukwa ni mkutano huohuo ndiyo ulimchagua Rais Samia kwa kura za ndio 1924 sawa na asilimia 100 kuwa mgombea wa kiti hicho cha urais.

Akitoa maelezo, alisema: “Tunafuta mgombea mwenza, lakini kama mnavyojua Dk Philip Mpango ndio Makamu wa Rais, amekuja kuniona kuniomba nimpumzishe, ana sababu kadhaa lakini sio za mahusiano ya kazi.”

“Anasema yeye ana miaka 68, angependa kuishi zaidi, ikiwezekana afikishe 90 huko, akasema mama yake amefika 80, nilimbishiabishia, wiki iliyopita akanikabidhi barua hii. Na barua sikumjibu. Nilipokwenda kuzungumza na kamati kuu tukakubaliana tumpumzishe.”

Leo Jumatatu Januari 20, 2025, Mwananchi Digital imezungumza na baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Songea mjini mkoani Ruvuma juu ya uteuzi huo huku wakisema chama hakijakosea, kimeteua mtu sahihi.

Sipilian Mapunda mkazi wa Songea mjini amesema Dk Nchimbi ni kiongozi sahihi, mzalendo, mchapakazi na asiyependa kuyumbishwa na mfuatiliaji wa mambo.

Hivyo, anasema Samia amepata mgombea mwenza makini na anayejua kusoma alama za nyakati na kufuatilia mambo chanya yanayoendelea nchini.

“Mimi naona uteuzi huu ni kwa chama, nchi, Watanzania na hata sisi wa mikoa ya kusini, ni mtoto wetu huyu, na alishawahi kuwa mbunge hapa, tunafahamu uchapakazi wake,” amesema Mapunda.

Naye mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Halima Hassan, Mkazi wa Mamanyigu Songea amesema, Wanasongea wanajivunia uwezo mkubwa alionao Dk Nchimbi akisema ni miongoni mwa viongozi wenye maono ya mikakati ya maendeleo.

"Ni chaguo bora kwa wakati sahihi, ametusaidia  wakulima wa  Songea kuinua uchumi wetu, alijitoa usiku na mchana kuhakikisha tunapata mbolea ya ruzuku akiwa mbunge wa jimbo hili na hata  ambao hatukuwa na uwezo alitununulia mbolea  na kutupatia  bure, ni imani yangu ataendeleza  mambo mema aliyofanya Songea kwa Watanzania wote,” amesema Hassan.

Mkazi mwingine, Keisha Tweve amesema ameupokea kwa furaha uteuzi wa Dk Nchimbi kuwa mgombea mwenza kwa sababu uwezo wake ni mkubwa.

“Huyu sasa akikaa na mama Samia pale juu, mambo yatakuwa mazuri sana, alipokuwa mbunge huku ametujengea shule ya Sekondari ya Dk Emmanuel Nchimbi kwa pesa zake binafsi, katusomeshea watoto wetu bure na wana kazi nzuri. Ni mtu mwema na mpenda haki,” amesema.


Naye Katibu wa Chama cha UND, Florence Nkale amesema CCM kumteua kuwa mgombea mwenza Nchimbi, hakijakosea, japo kuwa ni chama pinzani.


Mbio za ubunge

Historia inaonyesha mwaka 2005, Dk Nchimbi alirudi nyumbani kwao (Songea Mjini) kuanza harakati za kusaka ubunge baada ya chama chake kumteua rasmi.

Aliingia kwenye kinyang’anyiro hicho akipambana na Edson Mbogoro wa Chadema, aliyekuwa mpinzani wake mkuu.

Dk Nchimbi alisaidiwa na mtandao mkubwa wa CCM na kupata ushindi wa asilimia 67.6 dhidi ya asilimia 30.5 za Mbogoro.

Mara tu baada ya kuwa mbunge, Rais Kikwete alimteua kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, hii ilikuwa Januari 2006, alidumu kwenye wizara hiyo hadi Oktoba 2006 alipohamishiwa kwenye Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana,  hapa pia alikuwa Naibu Waziri tangu Oktoba 2006 hadi Februari 2008 kisha Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambako pia alikuwa Naibu Waziri hadi Novemba 2010.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Nchimbi alijitosa tena Jimbo la Songea Mjini. Kampeni za 2010 zilimnyima usingizi pamoja na kuwa chama chake kilikuwa kimechukua asilimia zaidi ya 90 ya vijiji, vitongoji na mitaa mwaka 2009.

Kama kawaida, alipambana tena na Mbogoro wa Chadema na kumshinda kwa mara ya pili, japo safari hii Dk Nchimbi akipoteza takriban ushindi wa asilimia 10 ukilinganisha na mwaka 2005. Katika uchaguzi huo, alipata asilimia 59.9 dhidi ya 37.48 za Mbogoro.