Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Telack amtwisha zigo la migogoro ya ardhi DC mpya Kilwa

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo akiapa.

Muktasari:

Amemtaka pia kujitahidi kwenda kusimamia mapato ya wilaya ipasavyo na kusimamia miradi ya Serikali ambayo Rais Samia ametoa fedha  nyingi katika miradi mabalimbali ya maendeleo.

Lindi. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainabu Telack amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo kuhakikisha anatatua changamoto ya migogoro ya ardhi kwa wakati na sio kukaa muda mrefu bila kutolea maamuzi.

 Akizungumza leo Alhamisi Machi 14, 2024 wakati wa kumuapisha kiongozi huyo  kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Telack amesisitiza kuwa Wilaya ya Kilwa ina  migogoro mingi ya ardhi ukiwemo wa Liwale pamoja na wa Kilwa.

"Wilaya ya Kilwa na Wilaya ya Liwale kuna migogoro ya ardhi, Kamishna wa ardhi ameshaanza kazi hivyo nikuombe Mkuu wa Wilaya kwenda kuusimamia ipasavyo mgogoro huo hadi umalizike,"amesema  Telack.

Amemtaka pia kujitahidi kwenda kusimamia mapato ya wilaya ipasavyo na kusimamia miradi ya Serikali ambayo Rais Samia ametoa fedha  nyingi katika miradi mabalimbali ya maendeleo.

Pia  amemtaka kwenda kufanya mikutano mara kwa mara ya wananchi na kutatua kero zao .

"Jitahidi kutatua migogoro mapema, usiende nayo taratibu na kama huwezi utawauliza wenzio waliotangulia. Pia kafanye mikutano mara kwa mara  na wananchi,”amesema.

 Telack amesema pia Wilaya ya Kilwa ina mifugo mingi  inayotoka sehemu mbalimbali na alishatoa maagizo kwa wafugaji wote kuchimba marambo, hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kumpa ushirikiano mkuu wa wilaya huyo ili agizo hilo litekelezeke.




Kwa upande wake,  Nyundo amemshukuru Rais Samia kwa kumuamini na kuhakikisha kuwa yale yote aliyoambiwa na mkuu wa mkoa atakwenda kuyafanyia kazi.

"Nimshukuru Rais Samia kwa kuniamini, niuhakikishie kuwa nitakwenda kufanyia kazi yote niliyoambiwa na sitamuangusha Rais ambaye amenipa dhamana ya kuiongoza Wilaya ya Kilwa."amesema Nyundo.