Tundu Lissu apigwa risasi Dodoma

What you need to know:

 

  • Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hali ya Tundu Lissu ni mbaya.

Dodoma. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi  na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.