Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Unavyoweza kutajirika kwa kuuza habari mitandaoni’

Muktasari:

  • Vyombo vya habari vimetakiwa kufanya utafiti wa habari na tabia za wasomaji ili kupata soko la wasomaji wa habari za mitandaoni.

Dar es Salaam. Wataalamu wa maudhui mitandaoni wamewashauri Watanzania kuacha dhana ya kupata taarifa za bure mitandaoni na badala yake walipie ili kupata kilicho bora.

Wameyasema hayo leo Februari 7, 2024 katika mjadala wa Mwananchi Space katika mtandao wa X, uliokuwa na mada isemayo ‘Bidhaa za maudhui mtandaoni zitakavyosaidia uendeshaji wa vyombo vya habari.’

Akichangia mada katika mjadala huo, mwanzilishi wa chaneli ya Simulizi na Sauti, Fredrick Bundala ameeleza jinsi mtandao wa Youtube ulivyobadilisha maisha yake tangu alipoacha kazi katika mtandao wa Bongo 5.

“Sehemu niyoliamua kujiajiri ilikuwa Youtube, nilianza polepole lakini kwa leo hii nimefanikiwa kuwa na kampuni yangu, nina vijana ambao tumeshirikiana pamoja, wanaendesha maisha yao na mimi naendesha maisha yangu kupitia Youtube zaidi,” amesema.

Amesema Youtube wana utaratibu unaoitwa Youtube Patner Program (YPP) ambao ili kuingizwa kwenye utaratibu wa malipo ni lazima uwe na watu 500 wanaokufuatilia na video unazoweka ziwe zimeangaliwa kwa mwaka mzima walau kwa saa 3,000.

“Ukiweza kufikisha hivyo vigezo, basi unaingia YPP, ukiingia maana yake yale matangazo yanayoonekana kwenye video unazotayarisha, Youtube wanawalipa watengeneza maudhui asilimia fulani, wanatoa asilimia 55 wao wanabaki asilimia 45,” amesema.

Hata hivyo, amesema inategemeana na watu wanaongalia video yako wapo wapi zaidi.

“Mfano video ikitazamwa zaidi Tanzania haiingiza fedha nyingi ukilinganisha na ikitazamwa Marekani.  Sisi asilimia 6 ya wafuatiliaji wetu ni wa Marekani, hawa ndiyo watu wanatupa kiwango kikubwa cha fedha kuliko wale wa hapa Watanzania,” amesema.

“Kwa Tanzania watazamaji 1,000 unapata labda dola senti 50 lakini kwa Marekani, Canada ukipata watazamaji 1,000 unaweza kupata dola za Kimarekani 5, 10 hadi 15,” amesema.

Kwa upande wake mdau wa habari Daudi Kosuri ameshauri kuwepo na maudhui ya kuvutia ili kuwavuta wasomaji mitandaoni.

“Kutokana na mabadiliko ya teknolojia yalinivuta kwenda kwenye maudhui ya mtandaoni, lakini ninachokutana nacho kwenye maudhui ya mtandaoni ndiyo kinanipa mashaka.

“Ukiingia kwenye mitandao ya vyombo vya habari unakutana na Copy and Paste (kuiga), habari ambayo uliiona kwenye gazeti unaikuta imebandikwa kama ilivyo kwenye mitandao yao,” amesema.

Amevitaka vyombo vya habari kufanya utafiti kabla ya kuingia kwenye biashara ya maudhui mitandaoni, ili kujua tabia na mazingira ya wasomaji wa habari hizo.

“Kwa sababu hawajafanya utafiti kujua chombo chao cha habari unakuta humo ndani wameiga aina ya uandishi wa chombo kingine, sisi watumiaji tunajiuliza niko sehemu sahihi au la.

“Ninachokiona maudhui mtandaoni ni biashara nzuri na waliotangulia wanafanya biashara ya kutosha, lakini hatujafanya utafiti kujua namna gani tunaweza kutumia hili,” amesema.