Vita dhidi ya Covid-19: Kwanini lazima Tanzania iungane kudhibiti maambukizi ya corona

Siku 17 baada ya Waziri Ummy Mwalimu kutangaza kuwa kila mtu anayeishi Tanzania achukue tahadhari dhidi ya virusi vya corona, mtu wa kwanza mwenye maambukizi aligundulika Machi 16.

Waziri huyo mwenye dhamana ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, aliitaka jamii kuepuka kushikana mikono, kukumbatiana na kupigana busu kama njia ya kuepuka kuambukizwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya la Dunia (WHO), virusi vya corona vinaambukizi kwa kuwa karibu na mtu mgonjwa na kuingiza mdomoni majimaji anayotoa wakati akikohoa au kugusa sehemu ambayo majimaji hayo yameangukia na baadaye kujishika usoni, puani au machoni.

Tamko lake liliitikiwa vizuri na vitendo vya viongozi wa kitaifa, walioonyesha njia mpya ya salamu katika vyombo vya habari, yakiwemo magazeti ya Mwananchi na The Citizen.

Kwanza, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alionekana katika picha akiwasalimu wafanyakazi wa ndege ya ATCL kwa kuwapungia mikono akiwa mbali, na siku mbili baadaye Rais John Magufuli alisalimiana na Maalim Seif Sharif Hamad kwa kugongana miguu. Pia, Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu na Gertrude Mongella walipigwa picha wakisalimiana kwa kugonganisha mikono.

Tahadhari hiyo ya waziri ya Februari 29, ilikuja siku 60 baada ya China kuitaarifu WHO kuwa imebaini “watu kadhaa wenye homa ya mapafu ambayo si ya kawaida katika jiji la Wuhan, lenye watu milioni 11 katika jimbo la Hubei”.

Januari 7, virusi vipya vilishatambuliwa. Kwa mujibu wa WHO, “virusi hivyo vipya vilipewa jina la 2019-nCoV” kutoka katika familia ya virusi vya corona. Familia hiyo pia ndiyo ina virusi vya Ugonjwa wa Mafua Makali (SARS) vilivyobainika mwaka 2003.

Baadaye WHO ilitangaza jina jipya kuwa Covid-19, “na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo kuitwa Virusi vya Mafua Makali 2 (SARS-CoV-2).

Machi 23, katika Ripoti ya Hali ya Covid-19 (63), WHO ilitangaza maambukizi kufikia 332,930, na vifo 14,510 katika nchi 162 na maeneo 25, huku China pekee ikiwa na maambukizi 81,601 na vifo 3,276. Cha kusikitisha, kulikuwa na maambukizi mapya 40,788 na vifo 1,727 ndani ya saa 24 (Machi 22) duniani. Wakati huohuo idadi ya maambukizi Tanzania ilifika 12, Kenya (15), Rwanda (17) na Uganda (1).

Machi 16, Waziri Mwalimu alitangaza kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza Mtanzania (46) aliyewasili kutoka Ubelgiji. Siku moja baadaye, Waziri Mkuu aliamuru kufungwa kwa shule kwa muda wa siku 30, (baadaye amri hiyo ikahusu vyuo vya elimu ya juu). Pia, Serikali ikapiga marufuku mikusanyiko, kama semina, warsha, ya kisiasa na ya michezo.

Sababu za corona kusambaa kwa kasi

Tofauti na magonjwa mengine ya mlipuko, kwa upande mmoja wataalamu wanasema Covid-19 inaambukiza kwa kasi, wakati kwa upande mwingine vyombo vya habari vimelikuza suala hilo.

Kitendo cha vyombo vya habari kulipa uzito suala hilo kuna faida na hasara kutegemeana na jinsi unavyoliangalia. Mwaka 1990 wakati Saddam Hussein alipoivamia Kuwait, rais wa wakati huo wa Marekani, George H. W. Bush, alifanikiwa kulishawishi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia azimio kwa sauti moja la kuilazimisha Iraq iwe imeondoe majeshi Kuwait ifikapo Januari 15, 1991.

Baadaye majeshi ya pamoja yalifanikisha azimio hilo. Ilikuwa wakati ambao matangazo ya moja kwa moja yalikuwa yakiongezeka kwa kasi. Kwa mara ya kwanza, mamilioni ya watu duniani yaliweza kushuhudia – mubashara – watangazaji kama Bernard Shaw wa CNN wakiripoti moja kwa moja kutoka eneo la vita huku makombora yakionekana katika anga la Iraq.

Desemba 2019, virusi hivyo vilishambulia. Tumo, si tu katika matangazo ya moja kwa moja, bali uandishi wa habari za kitakwimu (data journalism), akili ya kiteknolojia (artificial intelligence, AI) na mhemko wa mitandao ya kijamii. Kwa kuwa na AI, tunaweza kuchakata idadi kubwa ya taarifa kwa kufumba na kufumbua na ikakupa ramani ya dunia kuonyesha jinsi ugonjwa ulivyosambaa kwa wakati muafaka. Kwa kuwa na taarifa zote hizo si ajabu hofu.

Kwa upande mwingine, wataalamu wanazungumzia kasi ambayo virusi vya corona vinasambaa.

Kwa mujibu wa Profesa Mohammed Janabi, mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, ingawa Covid-19 inaua wastani wa asilimia 2 ya walioambukizwa, kiwango hicho ni hatari mara kumi kuliko aina nyingine ya mafua kama hatua za kujikinga hazifuatwi, na zaidi kwa mtu mmojammoja.

Kwa mujibu wa Jukwaa la Uchumi la Dunia (WEF) la Kujadili Hatua dhidi ya Covid, virusi vya corona vinasambaa kwa haraka zaidi kuliko vya Homa ya Mafua ya Mashariki ya Kati (MERS). Hata hivyo, takwimu za hivi karibuni zinaonyesha “si hatari kuliko SARS na MERS”.

Ndani ya wiki kadhaa, ilisema WEF, virusi hivyo “vimeshambulia watu wengi zaidi kuliko SARS ilivyofanya kwa miezi kadhaa, hali iliyosababisha WHO kutangaza mlipuko huo kuwa ugonjwa wa dunia. MERS, ambao ulianzia Saudi Arabia mwaka 2012, “ulichukua miaka nane kuambukiza watu 2,500.

Kwa kunukuu takwimu za hivi karibuni, WEF inasema kwa kila watu 50 walioambukizwa MERS, kiwango cha vifo ni watu 17, wakati SARS (5) na Covid-19 ni mmoja tu.

Hata hivyo, kuenea kwa magonjwa hayo kunaonyesha kuwa MERS ilichukua miaka 2.5 kuambukiza watu 1,000, wakati SARS siku 130, lakini Covid-19 imechukua siku 48 tu kufikia idadi hiyo ya maambukizi!

Kwa mujibu wa Al Jazeera, Januari 11, China ilitangaza kifo cha kwanza. Na katika Siku ya Wapendanao, Misri ikawa nchi ya kwanza barani Afrika kubaini mtu mwenye maambukizi, wakati barani Ulaya nchi ya kwanza kutangaza kifo ni Ufaransa.

Februari 29, Korea Kusini iliripoti idadi kubwa ya maambukizi wakati watu 813 walipogundulika, na kufikisha jumla ya watu 3,150 huku vifo vikifika 17. Pia Iran iliripoti kupaa kwa idadi ya maambukizi kutoka watu 388 hadi 593 katika muda wa saa 24, huku vifo vikifika 43.

Ilipofikia Machi 23, WHO ilirekodi vifo 3,276 nchini China, Misri (14) na Ufaransa (674). Wakati huo huo, nchini Korea Kusini, idadi ya vifo iliongezeka kutoka watu 17 hadi 111 na Iran kutoka 43 hadi 1,685 ndani ya siku 23! Kanda ya Afrika ilikuwa na maambukizi 990 na vifo 23. Italia, yenye maambukizi 59,138 ndiyo nchi iliyoathirika zaidi, ikiwa na vifo 5,476 (hadi Machi 23)!

Kujifunza katika mafanikio, makosa ya wengine

Hivi sasa nchi zinafanya kazi saa 24 kupunguza athari za Covid-19 – ambayo inatishia kutikisa uchumi wa dunia. Wachambuzi wanakubaliana kuwa njia bora ni kuchukua hatua mapema kwa kutathmini ukubwa wa tatizo na kuharakisha “kushusha urefu wa kichuguu” (flattening the curve).

Kwa kuangalia kwa haraka nini kimefanikiwa na nini hakijafanikiwa, unaziona nchi zilizofanikiwa kudhibiti kuenea, na nyingine hazijabahatika kufanikiwa.

Kwa mfano, ni wazi kuwa baadhi ya nchi zilizoathiriwa vibaya ama hazikuwa nyumbufu au hazikuwa na mikakati ya kutosha au vyote viwili, kwa dhana kwamba ni tatizo la “Uchina”. Athari zake zimekuwa mbaya kiafya, kiuchumi na kijamii.

Italia, sasa ndio nchi iliyoathirika zaidi, nje ya China. Ilikuwa na idadi kubwa ya vifo 795 kwa siku (Machi 21). Vilevile, Covid-19 imesambaa katika majimbo yote 50 ya Marekani, hali ambayo wachambuzi wanaihusisha na kiwango kidogo cha upimaji na kutochukua hatua mwanzoni. Machi 24, Kituo cha CNN kilitangaza maambukizi kufikia 48,807+ na vifo 611+, huku watu milioni wakizuiwa majumbani.

Kwa upande mwingine, Korea Kusini, ambayo ilikuwa na maambukizi mengi mwanzoni, ilifanikiwa kudhibiti kutokana na hatua ya kupima watu kwa wingi na kupunguza kuuenea.

Hali kadhalika, China ilichukua hatua madhubuti, ikiwa ni pamoja na kuzuia watu kutoka majumbani, pamoja na upimaji watu kwa wingi, jambo lililoshusha kwa haraka kasi ya kusambaa.

Mkakati wa Korea

Korea Kusini ililazimika kupambana na maambukizi 5,000 yanayohusishwa na kanisa la Shincheonji, ambako mwanamke mwenye umri wa miaka 61, ambaye alihudhuria ibada mara mbili kwa wiki – pamoja na waumini wengine 500 – aligundulika kuwa na maambukizi.

Mafanikio ya Korea Kusini yalitokana na mikakati ya kibunifu iliyohusisha upimaji wa watu ndani ya magari na ufuatiliaji wa eneo alipo mtu kwa njia ya mtandao (GPS), hivyo kupunguza foleni na mzigo kwa wahudumu wa afya.

Hadi wiki iliyopita, Korea Kusini, nchi yenye zaidi ya watu milioni 50, ilikuwa ikipima watu 5,200 kati ya wananchi milioni kulinganisha na Marekani yenye watu milioni 329 ambayo ilikuwa inapima watu 74 kati ya milioni, kwa mujibu wa tovuti ya Worldometer.com.

Kwa kutumia teknolojia ya GPS, serikali ya Korea Kusini iliweza kuonyesha alipo mtu mwenye maambukizi ya Covid-19 kupitia app maalum, hivyo kuutahadharisha umma kuepuka maeneo hayo.

Jingine muhimu, utengaji mzuri wa watu walioambukizwa pamoja na kufuatilia na karantini kwa watu waliokutana naye, ulianzishwa. Kwa wale ambao hawakupata maambukizi, kutekeleza vizuri maelekezo ya kutokaribiana (social distancing) kuliongeza nguvu katika mkakati wao.

Ingawa haikutangaza kuzuia watu kutoka majumbani, mseto wa hatua hizo ulipunguza maambukizi, hadi kufikia 147 Machi 20. Licha ya mafanikio hayo, Korea Kusini bado iko macho ikihofia maambukizi kurejea.

Mkakati wa China

Kwa upande mwingine, hatua ambazo China ilichukua ni pamoja na kuzuia watu kutoka nyumbani na kuweka vifaa vya upimaji, uwezo wa kulaza wagonjwa – ikiwa ni pamoja na jengo lenye vitanda 1,000 lililojengwa kwa siku sita, utekelezaji thabiti wa karantini.

Katika makala yenye kichwa kisemacho, Hatua Madhubuti za China Zimepunguza Kasi ya Virusi vya Corona. Zinaweza zisiwe fanisi Katika Nchi Nyingine, Kai Kupferschmidt na Jon Cohen wameandika: “Hospitali za China zilijaa wagonjwa wa Covid-19 wiki chache zilizopita na sasa ziko tupu”.

Mbali na kujenga hospitali, serikali ilipeleka madaktari katika jiji la Wuhan kutoka sehemu nyingine za nchi.

Ripoti ya pamoja ya wanasayansi ya WHO na serikali ya China iliyotoka Februari 28, ilisema mkakati madhubuti wa China – ambao pia ulihusisha ufuatiliaji wa kielektroniki – “ulidhibiti kasi ya kuenea”.

Pia China ilisimamisha michezo, kuongeza muda wa kufunga shule na kufuta sherehe za mwaka mpya. Kila aliyetoka, alilazimika kuvaa barakoa.

Mamlaka pia zilitumia app, hasa za AliPay na WeChat, kuhakikisha makatazo hayo yanatekelezwa.

Kwa mujibu wa Gabriel Leung wa Kitivo cha Tiba cha Li Ka Shing katika Chuo Kikuu cha Hong Kong, kupitia rangi (mithili ya taa za barabarani) katika simu za mkononi— ambazo ni kijani, njano au nyekundu kumaanisha hali ya afya ya mtu – walinzi katika stesheni za treni na vituo vingine walitambua nani wa kumzuia au kumruhusu apite.

“China inaweza kuwa ilitumia mpango kabambe, nyumbufu na thabiti ambao haujawahi kutokea katika historia,” ilisema ripoti hiyo.

Alipoulizwa inakuwaje Italia yenye watu milioni 60 ambayo kwa vifo imeizidi China yenye watu bilioni 1.3, Dk Mike Ryan, mkurugenzi mtendaji wa Programu ya Dharura ya WHO, alisema nchi zinatakiwa zifanye zaidi ya wananchi wake kutokaribiana.

Kila nchi ina mfumo wake wa afya. Ni muhimu kuwa na ufuatiliaji, alisema katika mazungumzo na CNN/ Facebook kuhusu Covid-19, kilichoendeshwa na Anderson Cooper na Dk Sanjay Gupta.

Kuzuia kuongezeka kwa maambukizi ni kwa kila Tanzania

Wakati tunaweza kuwa si Taifa lililoendelea kiteknolojia kama Korea Kusini, au kuwa na mipango mikali kama China, nguvu zetu zinaweza kuelekezwa katika kutumia uzoefu kutoka katika mikakati hiyo miwili na mingine mingi, kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo.

Kwa mujibu wa MedCram.com, timu ya wanasayansi kutoka vyuo na taasisi maarufu wanaochunguza “ustahimilifu wa virusi hewani na chini (aerosol and surface stability of the virus (SARS-Cov-2))” wamebaini kuwa baada ya kukohoa au kupiga chafya, virusi vinaweza kuonekana katika majimaji baada ya saa tatu, au saa nne katika shaba, au saa 24 katika mbao na hadi siku tatu katika plastiki au chuma kisichoshika kutu. Kitu muhimu si kutogusa vitu hivyo tu, bali kuvisafisha mara kwa mara.

Uamuzi wa Serikali kuzuia mikusanyiko, hivyo taasisi za elimu kufungwa nchi nzima saa 24 baada ya mtu wa kwanza kugundulika, ilikuwa hatua muhimu.

Taarifa kutoka kwa Waziri Mwalimu kwamba mara moja wataalam waliwafualitia watu waliokutana na wagonjwa mkoani Arusha na Dar es Salaam, ni uamuzi mwingine sahihi.

Na maagizo ya Rais Magufuli kwa kamati maalum inayoongozwa na Waziri Mkuu, akisaidiwa na Waziri wa Afya na wengine, kwamba wageni wote wanaoingia kutoka nchi zenye maambukizi ya corona, wajitenge kwa gharama zao kwa siku 14, kuzuia wanaotaka kwenda nchi hizo, kuimarisha maabara ya Taifa, kupeleka vifaa vya kupimia mipakani, kupunguza safari za ndani, na zaidi ya yote, kudhibiti upotoshaji na taarifa, yanaongeza nguvu katika kupunguza kasi ya maambukizi.

Changamoto inabakia katika uzingatiaji wa taratibu za usafi zilizoelekezwa katika usafiri wa umma, huduma na wananchi kutogusana. Hili linataka jitihada za kila mtu na nidhamu binafsi.

Kama Dk Jeff Pothof, wa Chuo Kikuu cha Wisconsin (UW Health) na ofisa anayehusika na afya na ubora wa usalama nchini Marekani alivyosema: “Kama tukifuata maelekezo ya kutokaribiana na ya usafi, itasaidia kupunguza kasi ya kusambaa kwa virusi ili kila anayetaka huduma, atibiwe.”

Lengo kubwa la kutokaribiana ni kupunguza kugusana na watu wanaoweza kuwa na maambukizi.

Itabidi kubadilisha jinsi watu na kampuni zinavyofanya kazi, jinsi ya kutekeleza shughuli zao za kila siku.

Jitihada za kutumia teknolojia kama ilivyoonyeshwa na mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Sadc ulioongozwa kutokea Dar es Salaam Ijumaa iliyopita, na mkutano kwa njia ya video kati ya Waziri Mkuu na viongozi, watendaji na waganga wakuu wa mikoa kutoka jijini Dodoma, unaonyesha haja ya kujikinga na kuhakikisha biashara zinaendelea.

Tayari kampuni, balozi na taasisi mbalimbali zinapunguza misongamano kwa baadhi ya shughuli ambazo si lazima kufika ofisini kufanyia nyumbani.

Kwa mtu mmojammoja, kuzuia kusambaza kunataka mimi na wewe kufanya kile tulicho na uwezo nacho; kuosha mikono au kutakatisha kila mara, kuzuia salamu za kushikana mikono, kuepuka mikusanyiko, busu, kukohoa na kupiga chafya ovyo.

Mtu anaweza kuuliza kwa nini tuhangaike wakati idadi ya maambukizi ni ndogo kuliko Ulaya au Marekani au kama awali nchini China?

Jibu ni rahisi. Kusipokuwa na hatua, tutakuwa na maambukizi mengi, (kurefusha kichuguu) na hali ikiwa mbaya, katika muda mfupi mfumo wetu utazidiwa.

Fikiria hospitali zenye uwezo wa kulaza wagonjwa 100 kwa siku. Zinaweza kulaza wagonjwa 10,000 kwa mwaka (siku 365). Hiyo ni wagonjwa 28 kwa siku. Lakini katika hali ambayo wagonjwa 10,000 wanatakiwa walazwe kwa miezi miwili (siku 60), hospitali zitakuwa zinapokea wagonjwa 167 kwa siku, yaani 67 zaidi ya uwezo. Hii ni hali ambayo hakuna nchi inataka iifikie. Na kwa kweli, hakuna anayetaka kuwa mgonjwa wa 101, achilia mbali 167!

Kwa bahati mbaya, jiji la Wuhan, Italia na Iran zilipitia au zinapitia hatua hiyo. Wachambuzi wanaonya kuwa Marekani inaelekea njia hiyo.

Ndio maana hatua zote zilizotangazwa na Serikali na kuchukuliwa na kampuni, na zaidi ya yote wewe binafsi, zitachangia kuzuia kiwango cha kusambaa kwa maambukizi ili kilingane na uwezo wetu wa kukimudu. Unaweza kupunguza kasi ya virusi. Kuwa sehemu ya kudhibiti. Chukua tahadhari zote muhimu. Fuata miongozo iliyotolewa na mamlaka. Na zaidi ya yote uwe na Imani.!

Imeandikwa na Bakari Machumu, Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti na Mwananchi Digital. Tweeter: @bmachumu, LinkedIn: Bakari Machumu, na kutafsiriwa na Angetile Osiah.

Waziri huyo aliitaka jamii kuepuka kushikana mikono, kukumbatiana na kupigana busu kama njia ya kuepuka kuambukizwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya la Dunia (WHO), virusi vya corona vinaambukizi kwa kuwa karibu na mtu mgonjwa na kuingiza mdomoni majimaji anayotoa wakati akikohoa au kugusa sehemu ambayo majimaji hayo yameangukia na baadaye kujishika usoni, puani au machoni.

Tamko lake liliitikiwa vizuri na vitendo vya viongozi wa kitaifa, walioonyesha njia mpya ya salamu katika vyombo vya habari, yakiwemo magazeti ya Mwananchi na The Citizen.

Kwanza, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alionekana katika picha akiwasalimu wafanyakazi wa ndege ya ATCL katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa kuwapungia mikono akiwa mbali, na siku mbili baadaye Rais John Magufuli alisalimiana na Maalim Seif Sharif Hamad kwa kugongana miguu. Pia, Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu na Gertrude Mongella walipigwa picha wakisalimiana bila ya kupeana mikono.

Tahadhari hiyo ya waziri ya Februari 29, ilikuja siku 60 baada ya China kuitaarifu WHO kuwa imebaini “watu kadhaa wenye homa ya mapafu ambayo si ya kawaida katika jiji la Wuhan, ulio na watu milioni 11 katikati ya jimbo la Hubei”.

Januari 7, virusi vipya vilishatambuliwa. Kwa mujibu wa WHO, “virusi hivyo vipya vilipewa jina la 2019-nCoV” kutoka katika familia ya virusi vya corona. Familia hiyo pia ndiyo ina virusi vya Ugonjwa wa Mafua Makali (SARS) vilivyobainika mwaka 2003.

Baadaye WHO ilitangaza jina jipya kuwa Covid-19, “na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo kuitwa Virusi vya Mafua Makali 2 (SARS-CoV-2).

Machi 21, katika Ripoti ya Hali ya Covid-19 (61), WHO ilitangaza maambukizi kufikia 266,073, na vifo 11,184 katika nchi 156 na maeneo 25, huku China pekee ikiwa na maambukizi 81,416 na vifo 3,261. Cha kusikitisha, kulikuwa na maambukizi mapya 32,000 na vifo 1,344 ndani ya saa 24 (Machi 20) duniani. Wakati huohuo hadi Jumapili ya Machi 22, idadi ya maambukizi Tanzania ilifika 12, huku Kenya (7) na Rwanda (11).

Katika matangazo ya moja kwa moja Machi 16, Waziri Mkuu alitangaza kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza Mtanzania mwenye umri wa miaka 46 aliyewasili kutoka Ubelgiji. Mara moja, Waziri Mkuu aliamuru kufungwa kwa shule kwa muda wa siku 30, ikiwa ni hatua ya kuzuia maambukizi (baadaye amri hiyo ikahusu vyuo vya elimu ya juu). Pia, Serikali ikapiga marufuku mikusanyiko, kama semina, warsha, ya kisiasa na ya michezo.

Sababu za corona kusambaa kwa kasi

Tofauti na magonjwa mengine ya mlipuko, kwa upande mmoja wataalamu wanasema Covid-19 inaambukizi kwa kasi, wakati kwa upande mwingine vyombo vya habari vimelikuza suala hilo.

Kitendo cha vyombo vya habari kulipa uzito suala hilo kuna faida na hasara kutegemeana na jinsi unavyoliangalia. Mwaka 1990 wakati Saddam Hussein alipoivamia Kuwait, rais wa wakati huo wa Marekani, George Bush (Sr), alifanya uhamasishaji wa kidiplomasia wa aina yake na kufanikiwa kulishawishi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia azimio kwa sauti moja la kuilazimisha Iraq iwe imeondoe majeshi Kuwait ifikapo Januari 15, 1991.

Baadaye majeshi ya pamoja yalifanikisha azimio hilo. Ilikuwa wakati ambao matangazo ya moja kwa moja yalikuwa yakiongezeka kwa kasi. Kwa mara ya kwanza, mamilioni ya watu duniani yaliweza kushuhudia – kwa utulivu kutoka sebuleni – watangazaji kama Bernard Shaw wa CNN wakiripoti moja kwa moja kutoka eneo la vita huku makombora yakionekana katika anga la Iraq.

Desemba 2019, virusi hivyo vilishambulia. Tumo, si tu katika matangazo ya moja kwa moja, bali uandishi wa habari za kitakwimu (data journalism), akili ya kiteknolojia (artificial intelligence, AI) na na mhemko wa mitandao ya kijamii. Kwa kuwa na AI, tunaweza kuchakata idadi kubwa ya taarifa kwa kufumba na kufumbua na ikakupa ramani ya dunia kuonyesha jinsi ugonjwa ulivyosambaa kwa wakati muafaka. Kwa kuwa na vyote hivyo, bila ya kuvidhibiti vizuri, inakuja hofu.

Kwa upande mwingine, wataalamu wanazungumzia kasi ambayo virusi vya corona vinasambaa.

Kwa mujibu wa Profesa Mohammed Janabi, mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, ingawa Covid-19 inaua wastani wa asilimia 2 ya walioambukizwa, kiwango hicho ni hatari mara kumi kuliko aina nyingine ya mafua kama hatua za kujikinga hazifuatwi, na zaidi kwa mtu mmojammoja.

Kwa nini? Kwa sababu inasambaa kwa kugusana na mgonjwa au mtu aliyebeba virusi, au kugusa eneo ambalo halijasafishwa kama vitasa na meza. Hadi sasa hakuna tiba, huku chanjo ikitarajiwa kupatikana baada ya miezi 18.

Kwa mujibu wa Jukwaa la Uchumi la Dunia la Kujadili Hatua dhidi ya Covid, virusi vya corona vinasambaa kwa haraka zaidi kuliko vya Homa ya Mafua ya Mashariki ya Kati (MERS). Hata hivyo, takwimu za hivi karibuni zinaonyesha “si hatari kuliko SARS na MERS”.

Ndani ya wiki kadhaa, ilisema WEF, virusi hivyo “vimeshambulia watu wengi zaidi kuliko SARS ilivyofanya kwa miezi kadhaa, hali iliyosababisha WHO kutangaza “mlipuko huo kuwa janga la dharura duniani”. Hiyo ni siku 30 baada ya China kuipa taarifa kuhusu virusi hivyo. Tangu wakati huo imeutangaza kuwa ugonjwa wa dunia.

MERS, ambao ulianzia Saudi Arabia mwaka 2012, “ulichukua miaka nane kuambukiza watu 2,500.

Kwa kunukuu takwimu za hivi karibuni, WEF inaona kuwa kasi ya vifo vinavyotokana na Covid-19 ni karibu asilimia 2.2, ingawa wataalamu wanasema unaweza kuzidi au kuwa chini ya hapo kwa kuangalia idadi ya maambukizi ambayo hayajathibitishwa. Lakini SARS imeua karibu asilimia 10 na MERS (35).

WEF inasema kwa kila watu 50 walioambukizwa MERS, kiwango cha vifo ni watu 17, wakati SARS ni watano na Covid-19 ni mmoja.

Kwa ulinganisho, kuenea kwa aina hizo tatu za virusi vya mafua kunaonyesha kuwa MERS ilichukua siku 903 au miaka 2.5 kuambukiza watu 1,000, wakati SARS siku 130) kuambukiza watu 1,000, lakini Covid-19 imechukua siku 49 tu kufikia idadi hiyo ya maambukizi!

Kwa mujibu wa Al Jazeera, jedwali la mlolongo wa matukio linaonyesha Januari 11, China ilitangaza kifo cha kwanza. Na katika Siku ya Wapendanao, Misri ikawa nchi ya kwanza barani Afrika kubaini mtu mwenye maambukizi, wakati barani Ulaya nchi ya kwanza kutangaza maambukizi ni Ufaransa.

Februari 29, Korea Kusini iliripoti idadi kubwa ya maambukizi wakati watu 813 walipogundulika, na kufikisha jumla ya watu 3,150 huku vifo vikifika 17. Pia Iran iliripoti kupaa kwa idadi ya maambukizi kutoka watu 388 hadi 593 katika muda wa saa 24, huku vifo vikifika 43.

Ilipofikia Machi 21, WHO ilikuwa imerekodi maambukizi 266,073 na vifo 11,184 kote duniani, huku China (vifo 3,261), Misri (7) na Ufaransa (450). Kama Korea Kusini, idadi ya vifo iliongezeka kutoka watu 17 hadi 102 na Iran kutoka 43 hadi 1,433 ndani ya siku 21! Wakati huo, Afrika ilikuwa na maambukizi 572 na vifo 12. Italia, yenye maambukizi 47,021 ndiyo nchi iliyoathirika zaidi, ikiwa na vifo 4,032 (hadi Machi 21)!

Kujifunza katika mafanikio ya wengine

Kwa nchi ambazo zinafanya kazi saa 24 kupunguza athari za Covid-19 – ambazo zinatishia kutikisa uchumi wa dunia, wachambuzi wanakubaliana kuwa njia bora ni kuchukua hatua mapema kwa kutathmini ukubwa wa tatizo na kuharakisha “kushusha urefu wa kichuguu”.

Kwa kuangalia kwa haraka nini kimefanikiwa na nini hakijafanikiwa, unaziona nchi zilizofanikiwa kudhibiti kuenea, na nyingine hazijabahatika kufanikiwa.

Kwa mfano, ni wazi kuwa baadhi ya nchi zilizoathiriwa vibaya ama hazikuwa nyumbufu au hazikuwa na mikakati ya kutosha au vyote viwili, kwa kuzingatia China iliyochukulia tatizo hilo kuwa la nchi. Athari zake zimekuwa mbaya kiafya, kiuchumi na kijamii.

Italia, sasa ndio ina tatizo kubwa nje ya China, ilikuwa na idadi kubwa ya vifo 7XX kwa siku (Machi 21). Vilevile, Covid-19 imesambaa katika majimbo yote 50 ya Marekani, hali ambayo wachambuzi wanaihusisha na kiwango kidogo cha upimaji na kutochukua hatua mwanzoni. Machi 21, Marekani ilikuwa na maambukizi xxx na vifo xxx, huku watu milioni xxx katika miji au majimbo xx wakizuiwa majumbani.

Kwa upande mwingine, hata hivyo, Korea Kusini, ambayo ilikuwa na maambukizi mengi mwanzoni, ilifanikiwa kudhibiti kutokana na hatua ya kupima watu kwa wingi ili kujua ukubwa tatizo na kupunguza kuuenea.

Hali kadhalika, China ilichukua hatua madhubuti, ikiwa ni pamoja na kuzuia watu kutoka majumbani, pamoja na upimaji watu kwa wingi, jambo lililoshusha kwa haraka kasi ya kusambaa.

Wiki mbili baada ya WHO kutambua virusi vya corona nchini China, ugonjwa huo ulishambaa kwa watu 550 na kuua 17, na kusababisha jiji la Wuhan liweke chini ya karantini pamoja na Xiantao na Chibi. Majiji mengi zaidi yaliwekewa amri ya kutotoka nyumbani baadaye.

Mkakati wa Korea

Korea Kusini ililazimika kupambana na maambukizi 5,000 yanayohusishwa na kanisa la Shincheonji, ambako mwanamke mwenye umri wa miaka 61, ambaye alihudhuria ibada mara mbili kwa wiki – pamoja na waumini wengine 500 – aligundulika kuwa na maambukizi.

Mafanikio ya Korea Kusini yalitokana na mikakati ya kibunifu iliyohusisha upimaji wa watu ndani ya magari na ufuatiliaji wa eneo alipo mtu kwa njia ya mtandao (GPS).

Kwa kutumia mfumo wa kupima watu wakiwa katika magari, ilipunguza foleni katika maeneo ya huduma za afya na mzigo kwa wafanyakazi wa afya.

Hadi wiki iliyopita, Korea Kusini, nchi yenye zaidi ya watu milioni 50, ilikuwa ikipima watu 5,200 kati ya wananchi milioni kulinganisha na Marekani yenye watu milioni 329 ambayo ilikuwa inapima watu 74 kati ya milioni, kwa mujibu wa tovuti ya Worldometer.com na Ofisi ya Sensa ya Marekani.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha CNN, kampuni ya teknolojia ya virusi ya Korea Kusini “ilibuni upimaji huo ndani ya wiki tatu, ikiunganisha watu waliokuwa wanataka kupima na maabara 96”.

Serikali ya Korea Kusini inasifika kwa kuwa na “uwazi wa taarifa”. Kwa mfano, kwa kutumia teklnolojia ya GPS kuonyesha alipo mtu mwenye maambukizi ya Covid-19 – imo katika app – serikali iliweza kuutahadharisha umma kumuepuka mtu huyo.

Jingine muhimu, utengaji mzuri wa watu walioambukizwa pamoja na kufuatilia na utaratibu karantini watu waliokutana naye, ulianzishwa. Kwa wale ambao hawakupata maambukizi, kutekeleza vizuri maelekezo ya kutokaribiana (social distancing) kuliongeza nguvu katika mkakati wao.

Ingawa haikutangaza kuzuia watu kutoka majumbani, mchanganyiko wa hatua hizo ulipunguza maambukizi, hadi kufikia 147 Machi 20. Licha ya mafanikio hayo, Korea Kusini bado haijawa salama kwa kuwa maambukizi yanaweza kurejea.

Mkakati wa China

Kwa upande mwingine, hatua ambazo China ilichukua ni pamoja na kuzuia watu kutoka nyumbani na kuweka vifaa vya upimaji, uwezo wa kulaza wagonjwa – ikiwa ni pamoja na jengo lenye vitanda 1,000 lililojengwa kwa siku sita, utekelezaji thabiti wa karantini.

Katika makala yenye kichwa kisemacho, Hatua Madhubuti za China Zimepunguza Kasi ya Virusi vya Corona. Zinaweza zisiwe fanisi Katika Nchi Nyingine, Kai Kupferschmidt na Jon Cohen wameandika: “Hospitali za China zilijaa wagonjwa wa Covid-19 wiki chache zilizopita na sasa ziko tupu”.

Mbali na kujenga hospitali, serikali ilipeleka madaktari katika jiji la Wuhan kutoka sehemu nyingine za nchi, ikiwemo timu ya watu 9,000 kutoka ndani ya jiji hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya wanasayansi ya WHO na serikali ya China iliyotoka Februari 28, mkakati madhubuti wa China – ambao pia ulihusisha ufuatiliaji wa kielektroniki – “ulidhibiti kasi ya kuenea kwa Covid-19”.

Pia China ilifanya vizuri katika suala la wananchi kutokaribiana wawapo pamoja, ikisimamisha michezo, kuongeza muda wa kufunga shule na kufuta sherehe za mwaka mpya, huku wengi wakifunga maduka. Kila aliyetoka, alilazimika kuvaa barakoa.

Mamlaka pia zilitumia app, hasa za AliPay na WeChat, kuhakikisha makatazo hayo yanatekelezwa. Ilifuatilia safari na hata kuzuia wenye maambukizi kusafiri.

Kwa mujibu wa mmoja wa wahusika katika mpango huo Gabriel Leung wa Kitivo cha Tiba cha Li Ka Shing katika Chuo Kikuu cha Hong Kong, “kila mtu ana aina fulani ya mfumo wa uongozaji (mithili ya taa za barabarani),”… namba za rangi katika simu za mkononi— ambazo ni kijani, njano au nyekundu humaanisha hali ya afya ya mtu, hivyo kuwawezesha walinzi katika stesheni za treni na vituo vingine kumtambua na kumruhusu apite.

Sehemu ya ripoti hiyo inasema: “China inaweza kuwa ilitumia mpango kabambe, nyumbufu na thabiti ambao haujawahi kutokea katika historia.

Alipoulizwa Italia, yenye watu milioni 60 ambayo kwa maambukizi imeizidi China yenye watu wengi kuliko nchi zote duniani (watu bilioni 1.3), Dk Mike Ryan, mkurugenzi mtendaji wa Programu ya Dharura ya WHO, alisema nchi zinatakiwa zifanye zaidi ya wananchi wake kutokaribiana.

Kila nchi ina mfumo wake wa afya. Ni muhimu kuwa na ufuatiliaji, alisema katika mazungumzo na CNN/ Facebook Coronavirus Global, kilichoendeshwa na Anderson Cooper na Dk Sanjay Gupta.

Kuzuia kuongezeka kwa maambukizi ni kwa kila Tanzania

Wakati tunaweza kuwa si Taifa lililoendelea kiteknolojia kama Korea Kusini, au kuwa na mipango thabiti kama China, nguvu zetu zinaweza kuelekezwa katika kutumia uzoefu kutoka katika mikakati hiyo miwili na mingine mingi, kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo.

Kwa mujibu wa MedCram.com, timu ya wanasayansi kutoka vyuo na taasisi maarufu wanaochunguza “ustahimilifu wa virusi hewani na chini (aerosol and surface stability of the virus (SARS-Cov-2))” wamebaini kuwa baada ya kukohoa au kupiga chafya, virusi vinaweza kuonekana katika majimaji baada ya saa tatu, au zaidi katika shaba, au wanaweza kuishi hadi saa 24 katika mbao na hadi siku tatu katika plastiki au chuma kisichoshika kutu. Kitu muhimu si kugusa vitu hivyo, bali kusafisha mara kwa mara.

Hadi hapo ni muhimu kukubaliana na uamuzi wa Serikali kuzuia mikusanyiko –hivyo taasisi za elimu kufungwa nchi nzima saa 24 baada ya mtu wa kwanza kugundulika.

Taarifa kutoka kwa Waziri Mwalimu kwamba timu imeundwa kufuatilia watu waliokutana naye mkoani Arusha na Dar es Salaam, ni uamuzi mwingine sahihi.

Na maagizo ya Rais Magufuli aliyotoa Jumapili iliyopita kwa kamati maalum inayoongozwa na Waziri Mkuu, akisaidiwa na Waziri wa Afya na wengine, kwamba wageni wote wanaoingia kutoka nchi zenye maambukizi ya corona, wajitenge kwa gharama zao kwa siku 14, kuzuia wanaotaka kwenda nchi hizo, kuimarisha maabara ya Taifa, kupeleka vifaa vya kupimia mipakani, kupunguza safari za ndani, na zaidi ya yote, kudhibiti upotoshaji na habari feki, yanaongeza nguvu katika kupunguza kasi ya maambukizi.

Changamoto inabakia katika uzingatiaji wa taratibu za usafi zilizoelekezwa katika usafiri wa umma, huduma na wananchi kutogusana. Hili linataka jitihada za kila mtu na nidhamu binafsi.

Kama Dk Jeff Pothof, wa Chuo Kikuu cha Wisconsin (UW Health) na ofisa anayehusika na afya na ubora wa usalama nchini Marekani alivyosema: “Kama tukifuata maelekezo ya kutokaribiana na ya usafi, itasaidia kupunguza kasi ya kusambaa kwa virusi ili kila anayetaka huduma, atibiwe.”

Lengo kubwa la kutokaribiana ni kupunguza kugusana na watu wanaoweza kuwa na maambukizi. zzzzzzz

Itabidi kubadilisha jinsi watu na kampuni zinavyofanya kazi, jinsi ya kutekeleza shughuli zao za kila siku ambako huhusisha kuridhisha nia, matamanio na mahitaji.

Jitihada za kutumia teknolojia kama ilivyoonyeshwa na mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Sadc ulioongozwa kutokea Dar es Salaam Ijumaa iliyopita, na mkutano kwa njia ya video kati ya Waziri Mkuu na wakuu, makatibu na waganga wakuu wa mikoa kutoka Mlimani jijini Dodoma, unaonyesha haja ya kujikinga na kuhakikisha biashara zinaendelea wakati wa ugonjwa huu ulioikumba dunia.

Kampuni, balozi na taasisi za kimataifa zinapunguza kugusana katika shughuli zao kwa wafanyakazi kufanyia nyumbani kazi ambazo si muhimu kufika ofisini.

Kwa mtu mmojammoja, kuzuia kusambaza kunataka mimi na wewe kufanya kile tulicho na uwezo nacho; kuosha mikono au kutakatisha kila mara, kuzuia salamu za kushikana mikono, kuepuka mikusanyiko, busu, kukohoa na kupiga chafya.

Kama meya wa Los Angeles, Eric Garcetti alivyoshauri umuhimu wa kuchukua hatua kujilinda na kuwalinda wapendwa wetu na majirani: “Tunaingia kipindi kigumu, hizi ni hatua za kutumia akili.”

Na hakuna anayefanya vizuri linapokuja suala la kutimiza wajibu wako, kuliko Dk Sanjay Gupta wa CNN alivyoshauri Wamarekani kutotoka nyumbani: “Fanya kama vile umebeba virusi vya corona.”

Tunaweza kupata funzo kwa kila mmoja. Mtu anaweza kuuliza kwa nini wakati idadi ya maambukizi ni ndogo kuliko Ulaya au Marekani au kama awali nchini China?

Jibu ni rahisi. Kusipokuwa na hatua, tutakuwa na maambukizi mengi, na hali ikiwa mbaya, katika muda mfupi mfumo wetu utazidiwa.

Fikiria hospitali zenye uwezo wa kulaza wagonjwa 100 kwa siku. Zinaweza kulaza wagonjwa 10,000 kwa mwaka (siku 365). Hiyo ni wagonjwa 28 kwa siku. Lakini katika hali ambayo wagonjwa 10,000 wanatakiwa walazwe kwa miezi miwili (siku 60), hospitali zitakuwa zinapokea wagonjwa 167 kwa siku, yaani 67 zaidi ya uwezo. Hii ni hali ambayo hakuna nchi inataka iifikie. Na kwa kweli, hakuna anayetaka kuwa mgonjwa wa 101, iwe huyo wa 167?

Kwa bahati mbaya, jiji la Wuhan, Italia na Iran zilipitia au zinapitia hatua hiyo. Cha kusikitisha, wachambuzi wanaonya kuwa Marekani inaelekea njia hiyo.

Ndio maana hatua zote zilizotangazwa na Serikali na kuchukuliwa na kampuni, na Zaidi ya yote wewe binafsi, zitachangia kuzuia kiwango cha kusambaa kwa maambukizi ili kilingane na uwezo wetu wa kukimudu. Unaweza kupunguza kasi ya virusi. Kuwa sehemu ya kudhibiti. Chukua tahadhari zote muhimu. Fuata miongozo iliyotolewa na mamlaka. Na Zaidi ya yote uwe na Imani.!

Machumuni ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd., chapishaji wa magaeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti na Mwananchi Digital. Follow him on Twitter: @bmachumu, LinkedIn: Bakari Machumu