Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adaiwa kumuua mwanaye bila kukusudia kisa soda

Picha ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya geita

Muktasari:

  • Mshtakiwa Stefano Mlenda anadaiwa kumpiga kwa fimbo  hadi kumuua mtoto wake baada ya kuiba Sh700  na  kununua soda

Geita.  Mkazi wa Kijiji cha Chigunga wilayani Geita, Stefano Mlenda(31)  amefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Geita  akishtakiwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia  mtoto Fredrick Stephano (7) baada ya kuiba Sh700 na kwenda kununua soda.

Kesi hiyo namba 12387 ya mwaka 2024 ilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Akisoma maelezo ya kosa mwendesha mashtaka wa Serikali,   Scollastica Teffe ameieleza Mahakama kuwa mstakiwa huyo anashtakiwa kwa kumuua Stephano bila kukusudia kinyume na kifungu cha 95 & 98 sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2022.


Mshtakiwa huyo anadaiwa  Novemba 16, 2023 alimpiga mtoto wake huyo kwa kwa kutumia fimbo mtoto baada ya  kuiba Sh700 na kutumia kiasi hicho cha fedha kununua soda.

Inadaiwa kuwa siku ya tukio alimkuta mtoto huyo akinywa soda eneo wanalouza vinywaji, alimchukua na kurudi naye nyumbani huku akimchapa kwa fimbo na alipofika nyumbani alimfunga mikono na miguu.

Wakili wa Jamhuri ameieleza Mahakama kuwa Novemba 17, 2023 mtoto huyo alifariki na mwili ulipofanyiwa uchunguzi wa kitaalamu ilibainika kifo cha mtoto huyo kimesababishwa na majeraha kwenye kichwa  na sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mshtakiwa huyo akiwa kwa mlinzi wa amani alikiri kuua bila kukusudia.

Hata hivyo, baada ya kusomewa maelezo ya awali mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi pale itakapopangwa tena.