Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aina mpya ya madini kutengenezea ‘mabawa’ ya ndege yagundulika Mtwara

Ofisa Madini wa Mkoa wa Mtwara, Mhandishi Ephraim Mushi akiwa ameshika baadhi ya madini ya jipsum yanayopatikana mkoani Mtwara. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Aina mpya ya madini yenye uwezo wa kutengeneza mabawa ya ndege, rangi za printer, rangi za nyumba na bidhaa nyingine nyingi yanayojulikana kama ‘Sand Beach Minerals’ yamepatikana katika Kata ya Msimbati Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Mtwara. Licha ya kuwepo kwa utajiri mkubwa wa gesi katika Mkoa wa Mtwara tafiti zimeonyesha kuwepo kwa madini mapya aina ya ‘Beach Sand Minerals’ yanayopatikana Mtwara katika Kata ya Msimbati.

Madini hayo ya mchanga wa bahari yanajumuisha uwepo wa madini saba ambayo ni Ilminate, Rutile, Zircon, Garnet, Sillimanite, Monazite na Leucoxene.

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake leo Ofisa Madini wa Mkoa wa Mtwara, Mhandishi Ephraim Mushi alisema kuwa tayari mwekezaji ameshapatiwa leseni za uchimbaji mdogo katika eneo hilo madini ambayo ni maarufu kama ‘Beach Sand Minerals’ ambayo pia yapo katika baadhi ya maeneo hapa nchini. 

Amesema kuwa Mtwara na tumepata pia madini hayo ambayo yakichimbwa yanaweza kuongeza hamasa ya uwekezaji katika mkoa wetu ambapo yanahitajika kwa wingi sokoni kutokana na mahitaji ya bidhaa zinazotengenezwa na madini hayo.

“Tunayo dhahabu, Madini ya ujenzi, viwandani, pia tunayo ya chumvi japo uzalishaji wa dhahabu ni mdogo kutokana na uwekezaji kuwa mdogo hata nguvu kazi sio ya kutosha,” amesema.

“Mwaka huu 2022/2023 tulipewa lengo la kukusanya Sh5 bilioni ambapo mpaka Mei mwaka huu tulikuwa tumekusanya zaidi ya Sh7 bilioni ambapo imetokana na uwepo usafirishaji wa makaa ya mawe na madini mengine,” amesema.

Bwana Ally Mbarak Nahdi  ambaye ni mwekezaji wa Madini Mapya Msimbati amesema kuwa madini hayo yana faida kubwa katika uwekezaji viwandani ambapo bado hayajaanza kuchimbwa.

“Haya madini ya mchanga wa bahari yana aina tatu za madini ndani yake ni mchanga ambao unatoka kwenye milima ya mbali sana na kituama kwenye bahari yaani ni 'Heavy Minerals,” amesema.

“Wakati wa uchimbaji unachukua mchanga unauchekeka na unapata vipande vidogo vyeusi ambavyo ndio madini yenyewe unaweza kutengenezea rangi za nyumba, plastic, karatasi, rangi za printer, mabawa ya ndege, dawa za mswaki, vipodozi na vingine vingi ambapo soko kubwa lipo nchini China,” amesema Nahdi.