Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Air France kuanza kutua Kilimanjaro Novemba

Muktasari:

  • Ujio wa ndege za Air France katika Uwanja wa KIA inatajwa kuongeza idadi ya watalii watakaoingia nchini kutalii kuanzia Novemba.

Dar es Salaam. Shirika la ndege la Ufaransa (Air France) linatarajia kuanza kuruka kati ya Paris-Charles de Gaulle na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) nchini Tanzania kuanzia Novemba mwaka huu.

Hatua hiyo inatajwa kuwa itaimarisha mawasiliano yake barani Afrika kama sehemu ya mkakati wa shirika hilo kupanua mtandao wake wa masafa marefu katika bara zima na kuboresha utoaji wa huduma kwa wasafiri wa kikanda.

Taarifa ya Air France inasema ndege itakayotumika katika safari hiyo ni aina ya Airbus A350-900 na itatua mara tatu kwa wiki siku za Jumatatu, Jumatano na Jumamosi zikitokea Paris na safari za kurudi kutoka Kilimanjaro siku za Jumanne, Alhamisi na Jumapili.

Aidha, safari hiyo inachukua nafasi ya safari ya Paris-Zanzibar-Dar es Salaam ambayo ilikuwepo awali.

"Ongezeko la njia ya Paris-Kilimanjaro ni uamuzi wa kimkakati unaolenga kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya kusafiri kwenda Afrika Mashariki," alisema Meneja mkazi wa Air France nchini Tanzania, Rajat Kumar.

Alisema safari hiyo mpya ni njia rahisi ya ufikiaji wa Mlima Kilimanjaro ambao ni maarufu nchini Tanzania, kilele cha juu zaidi barani Afrika na Tovuti ya Urithi wa Dunia wa Unesco.