Ajali yaua watu 10 Geita

Wednesday August 18 2021
lipic

Mkuu wa wilaya ya Bukombe, Said Nkumba

By Rehema Matowo

Bukombe. Watu 10 wamefariki dunia na nane kujeruhiwa baada ya gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kugongana uso kwa uso na gari la mizigo katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatano 18, 2021 katika kijiji cha Ilalwe kata ya Bukombe wilayani Bukombe na kuhusisha gari la jeshi lililobeba ndugu waliotoka kwenye msiba wilaya ya Kahama likigongana na gari ya mizigo.

Mkuu wa wilaya ya Bukombe, Said Nkumba amesema hadi sasa majeruhi Sita wamewahishwa katika hospitali ya Ushirombo na wawili wapo kituo cha afya Masumbwe.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya hadi sasa taarifa aliyopokea miongoni mwa marehemu yupo mwanajeshi mmoja.

Miili ya waliopoteza maisha imehifadhiwa hospitali ya Masumbwe na chanzo cha ajali bado hakijafahamika na jeshi la polisi linandelea na uchunguzi kwenye eneo la tukio.

Advertisement