Ajali yaua watu watano Handeni

Saturday November 21 2020
ajali pic
By Rajabu Athumani

Handeni. Watu watano wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya magari mawili ya mizigo kugongana uso kwa uso wilayani Handeni mkoani Tanga alfajiri ya leo Jumamosi Novemba 21, 2020.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Kitumbi na kuhusisha magari aina ya kenta na lori ambayo yaliwaka moto baada ya kugongana.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda amesema kila gari lilikuwa na watu watatu na baada ya ajali watano walifariki dunia papo hapo na mmoja amejeruhiwa.

 “Ajali imetokea eneo la Kitumi kabla ya Mkata, gari aina ya Toyota kenta  ilikuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Lushoto na lori lilikuwa linatoka Tanga kwenda Dodoma. Yalikutana uso kwa uso lakini magari yote mawili yaliwaka moto na kusababisha vifo vya watu watano.

“Watu watatu waliokuwa kwenye kenta walipoteza maisha na waliokuwa kwenye lori wawili walipoteza maisha na mmoja amejeruhiwa na amelaza katika kituo cha afya cha Mkata anakoendelea na matibabu,” amesema kamanda huyo.

Advertisement
Advertisement