Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyekuwa Kocha Simba, wenzake waburuzwa kortini

Muktasari:

  • Aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya Simba, Muharami Sultan na wenzake watano wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine.

Dar es Salaam. Watu sita akiwemo aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya Simba, Muharami Sultan (40) wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za Kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilogramu 34.89.

Washtakiwa wengine ni mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zubery Seif, Said Matwiko mkazi Magole, Maulid Mzungu maarufu mbonde (54), mkazi wa kisemvule, John John ‘Chipanda’ (40) mkazi wa Kitunda na Sarah Joseph.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Grace Mwanga alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mery Mrio kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mshtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya.

Mwanga alidai Oktoba 27,2022 eneo la Kivule jijini Dar es Salaam washtakiwa wote kwa pamoja walisafirisha dawa za Kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilogramu 27.10.

Alidai katika shtaka la pili Novemba 4,2022 maeneo ya Kamegele Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani washtakiwa hao kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilogramu 7.79.

Upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo aliomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine na ada ya maelezo hayo Hakimu Mrio alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na washtakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote na kesi imeahirishwa hadi Desemba 5,2022.