Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyeua bila kukusudia aachiwa huru

Watu saba wafikishwa kortini wakidaiwa kujipatia Sh 428milioni mali ya Tanesco

Muktasari:

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema mshtakiwa huyo baada ya kumjeruhi marehemu, alijutia itendo ulichokifanya na alitumia nguo yake kumfunga kwenye jeraha ili kumfikishwa hospitalini.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia mkazi wa Manzese, Yasir Khalfan kwa masharti ya kutofanya kosa lolote na atakuwa kwenye uangalizi ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Hukumu hiyo imetolewa leo Septemba 2 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi akisema baada ya mshtakiwa huyo kukubali kosa la kuua bila ya kukusudia mahakama hiyo ilimtia hatiani.

Amesema mshtakiwa huyo baada ya kumjeruhi imarehemu inaonekana ulijutia kitendo ulichokifanya ulichana nguo yake na kumfunga kwenye jeraha na ulimsaidia kumfikishwa hospitalini.

"Haya yanaashiria kwamba dhamira yako haikua ovu pia umri wa miaka 21 ulikouwa nao wakati unafanya kosa kilikua ni kipindi cha kuonesha msuli, ni kipindi ambacho siyo cha kutumia busara," amesema Shaidi.

Awali wakili wa Serikali, Mwanahamina Kombakono akimsomea maelezo ya mshtakiwa huyo, amesema Machi 12, 2015 akiwa eneo la Manzese Madizini wakicheza Kamari na marehemu Adam, kulitokea kutoelewana kati ya mshtakiwa na marehemu huyo ambapo mshtakiwa alikuwa akimdai pesa ambazo marehemu alikataa kumlipa.


Khalfan akiwa ana mdai marehemu huyo, ghafla alisukumwa kwa ishara ya kumpiga ndipo alichukua kisu na kumchoma shingoni na baada ya kumjeruhi akiwa anavuja damu nyingi mshtakiwa huyo alichana shati lake na kumfunga ili damu zisiendelee kutoka huku akiwa na watu wengine walimsaidia kumkimbiza hospitalini na alipofika alifariki dunia

Kombakono anadai hospitali ilifanya uchunguzi ilidaiwa kuwa marehemu alifariki kutokana na kuvuja damu nyingi.

Baada ya kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo alikubali kutenda kosa hilo.

Naye wakili wa utetezi, Harrison Lukosi aliieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa ni mkosaji kwa mara ya kwanza na kwa kuangalia mazingira ya kutendeka kosa hili mshtakiwa alifanya jitihada kuokoa uhai wa marehemu ikiwemo kuzuia asiendee kupoteza damu.