Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amchoma mke wake kisu kwa wivu wa mapenzi

Muktasari:

Mkazi wa Kijiji cha Mbalibali Wilaya ya Serengeti, Mary Julius (22) amenusurika kufa baada ya kuchomwa kisu kwenye titi na mume wake, Mussa Samwel chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Serengeti. Mkazi wa Kijiji cha Mbalibali Wilaya ya Serengeti, Mary Julius (22) amenusurika kufa baada ya kuchomwa kisu kwenye titi na mume wake, Mussa Samwel chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Oktoba 11, 2021 mchana nyumbani kwao baada ya mume kumkuta mke wake akiongea na simu.

Mmoja wa wanafamilia amesema mtuhumiwa alimkuta mke wake ndani akiwa anaongea na simu akaanza kumshambulia kwa matusi kisha akamchoma kisu akimtuhumu kuwa alikuwa anaongea na hawara wake.

"Baada ya kumchoma mke wake akaanguka tulifika eneo la tukio na kumkamata huku wengine wakimkimbiza majeruhi hospitali ya wilaya akiwa katika hali mbaya sana," amesema mmoja wa familia ambaye jina lake limehifadhiwa.

Taarifa zinasema kuwa baada ya Mary kuchomwa kishu alipelekwa katika katika Hospitali ya Wilaya ya Serengeti huku hali yake ikiwa mbaya.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti, Antonita Zephania amesema majeruhi amefkishwa akiwa katika hali mbaya.

"Tulimpiga Utra sound ili tumebaini kisu hakikufika kwenye moyo, tumemhudumia na amelazwa akiendelea na matibabu, kwa kifupi aliumizwa sana," amesema.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishibwamu kuthibitisha tukio hilo hakupokea simu, lakini taarifa za polisi wilayani humo zinasema mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha polisi Mugumu.