Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anayedaiwa kuiba mita za maji aendelea kusota rumande

Muktasari:

  • George anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kudaiwa kuiba mita, kusabisha hasara na kuharibu miundombinu ya kutoa huduma ya maji.

Dar es Salaam. Serikali imesema bado inaendelea na uchunguzi katika kesi ya kuiba mita za maji inayomkabili mfanyabiashara Daud George (28).

George,mkazi wa Kinondoni anakabiliwa na mashtaka matatu, likiwemo la kuiba mita za maji na kuisababishia hasara ya Sh 904,277 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa).

Wakili wa Serikali, Erick Kamala, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne, Januari 21, 2025, wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi ilipoitwa kwa kutajwa: "Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa kesi hii bado unaendelea, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amesema Kamala.

Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, ameahirisha kesi hadi Februari 3, 2025 kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa yupo rumande.

Kesi hiyo imesikilizwa kwa njia ya video, huku mshtakiwa akiwa gerezani.

Hata hivyo, hakimu Mwankuga amemuelekeza mshtakiwa huyo kuwa dhamana yake ipo wazi, anatakiwa atafute wadhamini ili tarehe ijayo aletwe mahakamani kupewa masharti ya dhamana.

Kwa mara ya kwanza, mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo Januari 8, 2025, na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu.

Katika shtaka la kwanza, ambalo ni kuharibu miundombinu ya kutoa huduma muhimu, anadaiwa Novemba 18, 2024, katika mtaa wa Mwananyamala Sindani, aliharibu mita tatu zinazotumiwa kupima kiasi cha maji yanayotumika, mali ya Dawasa.

Shtaka la pili, siku na eneo hilo, George alidaiwa kuiba mita tatu za maji zenye thamani ya Sh 904,277 mali ya Dawasa.

Shtaka la tatu, siku na eneo hilo, mshtakiwa aliisababishia hasara Dawasa ya Sh 904,277 kwa kitendo hicho.