Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anayedaiwa kumuua Angela mikononi mwa Polisi

Marehemu Angela Stephano (aliyepo nyuma) akiwa kwenye picha ya pamoja na mama yake mzazi, Mary Msuya enzi za uhai wake.

Muktasari:

  • Tukio hili liliripotiwa na Mwananchi Agosti 9 mwaka huu na mama mzazi wa marehemu Angela, Mary Msuya alisema alipata hofu juu ya afya ya mwanawe baada ya kumpigia simu.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi linamshikilia mtu mmoja Jackson Magoti (34) kwa tuhuma za kufanya mauaji ya Angela Joseph (23) mkazi wa Michese jijini Dodoma chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hili liliripotiwa na Mwananchi Agosti 9 mwaka huu na mama mzazi wa marehemu Angela, Mary Msuya ambapo alisema alipata hofu juu ya afya ya mwanawe baada ya kumpigia simu.

"Nilimpigia simu hakupokea lakini akanijibu kwa SMS (ujumbe mfupi wa maneno) kuwa mama bwana tu- chat simu yangu ni mbovu. Nikamwambia mtoto anaumwa akanitumia Sh25,000 ilikuwa ni Jumamosi (Julai 20, 2024),” alisema.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime leo Agosti 25, 2024,  Angela alikutwa ameuawa Agosti 21, mwaka huu Saa 7:45 mchana na mwili wake kufungwa ndani ya boksi kisha kutumbukizwa kwenye kiroba na kutupwa kichakani.

Amesema mama wa binti huyo alianza kumtafuta baada ya kutomuona tangu Julai 22, 2024 hivyo polisi walianza uchunguzi, ilipofika Agosti 11, mwaka huu walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Magoti.

"Uchunguzi umebaini chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi," amesema Misime.

Mbali na tukio hilo, Misime amesema  wanafanya uchunguzi wa tukio lingine la mauaji ambalo mtuhumiwa aliwahi kutenda la kumuua binti mmoja mfanyakazi wa kazi za ndani jijini Mwanza, ambalo lilitolewa  taarifa na jeshi hilo Agosti 23, mwaka huu.

Pia jeshi hilo linamshikilia Elias Chimuse (33), Mkazi wa Ibihwa, wilayani Bahi, Mkoa wa  Dodoma na wenzake 11 kutokana na tuhuma za mauaji yaliyotokea Agosti 10 , 2024 saa mbili usiku katika Kijiji cha Ibihwa.

Amesema watuhumiwa hao 11 watafikishwa mahakamani kwa kosa la kuua watu wawili na kisha kuwachoma moto pamoja na gari walilokuwa wanalitumia lenye namba za usajili T583 BEW aina ya Toyota Cresta.

Mbali na matukio hayo, jeshi hilo pia linamshikilia Samwel Chiwalanga (42) Mkazi wa Chang'ombe Extensio, Dodoma na Tabata, Dar es Salaam kwa tuhuma za kujifanya Ofisa wa Usalama wa Taifa Ikulu na kuwatapeli viongozi wa umma wa kada tofauti.

"Mtuhumiwa amekuwa akiwatapeli viongozi wa umma na kada tofauti kwamba ana uwezo wa kuwapandisha vyeo au kuwabadilisha nafasi za kazi lengo likiwa ni kujipatia fedha," amesema.

Misime amesema mtuhumiwa huyo alikutwa na kitambulisho cha kughushi cha idara ya Usalama wa Taifa na silaha aina ya bastola aliyokuwa anaimiliki kinyume cha sheria.