Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anayedaiwa kuvunjwa miguu na Polisi afanyiwa upasuaji Bugando

Mohammed Khatibu akiwa amelala kitandani nyumbani kwao Kirumba anakouguza majeraha yaliyotokana na kipigo anachodaiwa kupata kutoka kwa Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kiseke Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Paulo Mbegete. Picha na Mgongo Kaitira. 

Muktasari:

Mkazi wa Mtaa wa Mlimani'A' eneo la Kabuoro kata ya Kirumba wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Mohammed Khatibu anayedaiwa kuvunjwa miguu kwa kipigo akiwa kituo cha polisi amefanyiwa upasuaji.

Mwanza. Mohamed Khatibu (29), mkazi wa Mtaa wa Mlimani 'A' eneo la Kabuoro Wilayani Ilemela mkoani Mwanza anayedaiwa kuvunjwa miguu kwa kupigo akiwa Kituo Kidogo cha Polisi Kiseke amefanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Februari 13, 2023.

Kijana Mohamed ambaye ni dalali wa magari jijini Mwanza anadaiwa kushushiwa kipigo na Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kiseke Wilaya ya Ilemela, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Paulo Mbegete kwa madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mazazi mwenzake.

Tukio hilo lilitokea Januari 3, 2023 baada ya kukamatwa na kiongozi huyo wa Polisi anayedaiwa kushirikiana na rafiki yake ambaye hadi sasa hajafahamika. Mtuhumiwa huyo tayari ametiwa mbaroni.

Kutokana na madhara hayo ya kiafya, Mohamed aliyefikishwa Hospitali ya Bugando kwa mara ya kwanza Januari 3, 2023 amelazimika kufanyiwa upasuaji kurekebisha mifupa na viungo vilivyoathiriwa na kipigo hicho.

Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni akiwa amelala kitandani nyumbani kwao Kirumba anakoendelea kuuguza majeraha, Mohamed amesema upasuaji huo uliogharimu zaidi ya Sh1.2 milioni ulifanyika kwa ufanisi Februari 13, 2023.

"Naushukuru uongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kuonyesha kuguswa na tukio langu kwa kushirikiana na familia yangu katika hatua mbalimbali kuhakikisha napata matibabu,” amesema Mohamed ambaye sasa analazimika kutembelea magongo

Kijana huyo pia amewashukuru madaktari, wauguzi na watumishi wote wa Hospitali ya Bugando kwa huduma nzuri wanayompatia ikiwemo kurekebisha vikombe vya magoti yake vilivyobainika kupasuka kwa kipigo.

“Nimeanza kufanya mazoezi mepesi kurejesha utimamu wa viungo vyangu baada ya upasuaji,” amesema Mohamed akionyesha tabasamu la matumaini

Akizungumzia hali ya afya ya mtoto wake, Hidaya Somba, mama mzazi wa Mohamed ameushukuru uongozi wa Jeshi la Polisi, Madaktari wa Hospitali ya Bugando na wote walioshirikiana na familia kufanikisha gharama za matibabu.

Mohammed Khatibu akiwa amelala kitandani nyumbani kwao Kirumba anakouguza majeraha yaliyotokana na kipigo anachodaiwa kupata kutoka kwa Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kiseke Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Paulo Mbegete. Picha na Mgongo Kaitira. 


“Ofisi ya RPC (Kamanda wa Polisi Mkoa) na RCO (Mkuu wa Upelelezi Mkoa) wa Mwanza imetoa ushirikiano wa kutosha kuanzia kumsaka na kumtia mbaroni mtuhumiwa na kuchangia baadhi ya gharama za matibabu. Kwa kweli tunaushukuru sana uongozi wa Jeshi la Polisi Mwanza,” amesema Hidaya.