Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Apigwa risasi akijaribu kuwatoroka polisi

Muktasari:

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo ni kati ya  watano waliokamatwa kwa tuhuma za  kuvamia maduka makubwa na kupora mali jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi mguuni na polisi wakati akijaribu kuwatoroka.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo ni kati ya  watano waliokamatwa kwa tuhuma za  kuvamia maduka makubwa na kupora mali jijini Dar es Salaam.

Sirro alisema tukio hilo lilitokea Septemba 14 eneo la Ununio wakati mtuhumiwa akiwapeleka polisi kuwaonyesha ilipokuwa imefichwa silaha  kwenye majaruba ya chumvi.

Alisema mtuhumiwa alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali kwa matibabu kutokana na kutokwa damu nyingi.

Awali, alisema watuhumiwa hao, akiwamo mwanamke, walikamatwa katika eneo la Goba na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na matukio hayo.