Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ashambuliwa hadi kufa akituhumiwa kuiba mahindi

New Content Item (1)

Muktasari:

Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti yaliyotokea mkoani Shinyanga hivi karibuni, likiwemo la mwanaume aliyeshambuliwa hadi kufa akidaiwa kuiba mahindi mabichi shambani.

Shinyanga. Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti yaliyotokea mkoani Shinyanga hivi karibuni, likiwemo la mwanaume aliyeshambuliwa hadi kufa akidaiwa kuiba mahindi mabichi shambani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu amewataja watu hao kuwa ni Tumaini Malima (35) mkazi wa mtaa wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga na mwanaume mwingine ambaye hajafahamika anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 35 hadi 40.

Alisema mtu huyo ambaye hajatambulika jina wala makazi yake ameuawa kwa kushambuliwa na wananchi kwa tuhuma za kuiba mahindi shambani katika kijiji cha Mwamalili kilichopo Manispaa ya Shinyanga huku Tumaini akifariki wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Mwawaza baada ya kujeruhiwa na jiwe alilopigwa na Yohana Daniel akiwa baa ya Heinken mjini Shinyanga.

Ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa jeshi hilo pindi matukio ya uhalifu yanapotokea.