Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asimulia kuaacha kuvuta bangi akihofia kurudi jela mara ya tatu

Muktasari:

Kijana mmoja mkazi wa Mikindani mkoani Mtwara, Seif Libaba amesema kuwa amelazimika kuacha kutumia dawa za kulevya baada ya kuishi kwa hofu ya kukamatwa mara kwa mara na kufungwa jela kwa zaidi miaka mitatu.


Mtwara. Kijana mmoja mkazi wa Mikindani mkoani Mtwara, Seif Libaba amesema kuwa amelazimika kuacha kutumia dawa za kulevya baada ya kuishi kwa hofu ya kukamatwa mara kwa mara na kufungwa jela kwa zaidi miaka mitatu.

Akizungumza kwenye mahojiano na Mwananchi  amesema kuwa dawa hizo alianza kutumia tangu akiwa shule ya sekondari kwa kushawishiwa na marafiki zake.

“Niliona matumizi hayana faida kwangu nilianza kutumia dawa za kulevya nikiwa nasoma shule ya sekondari. Tulikuwa tunavuta hadi bangi, lakini hakuna yalichonisaidia zaidi ya kuwa duni kila siku huku afya yangu ikidhoofu.

“Nilihama Mtwara nikienda Dar es Salaam hapo nilikuta kundi kubwa la vijana wakitumia, nilianza kutumia na mimi kwa kufuata marafiki ambapo walianza kuninulia wao mwishoni nikaanza mimi kununua na kutumia mwenyewe,” amesema.

“Nilijutia sana maisha yangu yaribika kila siku nilikuwa naenda jela hali ambayo ilichangia mimi kuacha kabisa kutumia dawa hizo. Ukianza kutumia ni mtihani mgumu sana ni vyema mtu akiacha,” amesema.

“Kuna wakati nilikamatwa nilifungwa jela miaka mitatu lakini niliporudi uraiani bado niliendelea kutumia hali ambayo ilipeleka mimi kukamatwa tena na kurejeshwa jela kwa mara ya pili,” amesema.

Mratibu wa Afya ya Akili wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Koletha Mnunduma alisema kuwa kati ya waathirika 88 wanawake 24 na wanaume wakiwa ni 64.

“Tumekuwa tukitoa elimu na dawa katika Kitengo cha Dawa za Kulevya  ambapo watu 42 walipona na kati ya  hao 7 ni wanawake huku wengine wakiwa na nafuu kubwa,” amesema.