Askari Mkomazi auawa na nyati
Muktasari:
- Askari wa Uhifadhi, katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Samwel Edward Nassari amefariki dunia baada ya kugongwa na Nyati katika eneo la Mbula lilipo katika hifadhi hiyo, Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.
Same. Askari wa Uhifadhi, katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Samwel Edward Nassari amefariki dunia baada ya kugongwa na nyati katika eneo la Mbula lilipo katika hifadhi hiyo, wilayani ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamishna Msaidizi Hifadhi ya Mkomazi, Emmanuel Moirana amesema tukio hilo limetokea leo Jumanne Agosti Mosi, 2023 wakati askari huyo akitekeleza majukumu yake.
"Mtumishi mwenzetu amefariki leo baada ya kugongwa na nyati wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kazi," amesema Moirana
Naye Kamishna wa Uhifadhi Tanapa, William Mwakilema ametuma salamu za pole kwa familia, watumishi wote wa Jeshi la Uhifadhi, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha askari huyo.