Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Konki: Miaka 75 ya Elim Tanzania imetukomaza

Waziri wa Madini, Dotto Biteko (wapili kulia) ambaye amemwakilisha Makamu wa Rais Dk Philip Mpango kwenye maadhimisho ya Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa la Elim Tanzania, yaliyofanyika mjini Babati mkoani Manyara, kulia kwake ni Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Peter Konki. Picha na Joseph Lyimo

Muktasari:

Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania linaadhimisha Jubilee ya miaka 75 baada ya kuanza kutoa huduma yake Tanzania mwaka 1946

Babati. Askofu Mkuu wa Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania, Peter Konki amesema miaka 75 ya uwepo wa Kanisa hilo imewakomaza katika kutoa huduma ya kiroho na kimwili kwa Watanzania.

 Askofu Konki ambaye pia ni Mwenyekiti wa makanisa ya pentekoste Tanzania (CPCT) ameyasema hayo leo Jumapili Septemba 25, 2022 mjini Babati mkoani Manyara, kwenye maadhimisho ya Jubilee ya miaka 75 ya kanisa la Elim.

Amesema katika kuadhimisha Jubilee ya miaka 75 ya kanisa hilo wamefanikisha maendeleo mbalimbali ikiwemo kujenga makanisa, majengo ya wachungaji, kutoa elimu na huduma nyingine.

Amesema katika kutumikia kanisa la Elim Tanzania amedhamiria kuhakikisha kanisa jipya linajengwa mjini Babati litakalogharimu Sh800 milioni.

"Kanisani ni mahali pakutoa faraja kwa kila mwenye huzuni, wagonjwa kupona, kufungisha ndoa na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii," amesema Askofu mkuu Konki.

Waziri wa Madini, Dotto Biteko amempongeza Askofu Konki kwa kuongoza ipasavyo kanisa hilo kwani miaka 75 ni mingi katika kutoa huduma nchini.

"Askofu Mkuu Konki tunakupongeza mno kwani nguvu ya kiongozi ndiyo nguvu ya kanisa na jeshi la kondoo linaloongozwa na simba ni imara kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo," amesema Waziri Biteko.

Askofu wa Calvary Assemblies of God, Dk Dastan Maboya amesema Elim Pentekoste Tanzania ni miongoni mwa kanisa kongwe linalotoa huduma za kiroho.

Askofu Simon Githigi wa Elim Pentekoste Kenya ambaye ni Mwenyekiti wa makanisa ya Elim Pentekoste Afrika amesema kanisa hilo lilianzishwa Uingereza mwaka 1915.