Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Shoo atoa ujumbe kwa vijana

Baadhi ya vijana wa KKKT kutoka Dayosisi 27 nchini katika ufungaji kongamano la vijana mjini Tabora. Picha na Robert Kakwesi

Muktasari:

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo leo Jumatatu amefunga Kongamano la vijana wa kanisani hilo lilianza Agosti 9, 2022 likihusisha vijana 540 lililofanyikia Mkoa wa Tabora.

Tabora. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo amewataka vijana wa nchini humo kujituma katika kufanya kazi kwa vile wanategemewa na kanisa na Taifa kwa ujumla.

 Askofu Shoo amesema hayo leo Jumatatu, Agosti 15, 2022 wakati akifunga kongamano la vijana wa kanisa hilo linalofanyikia Mkoa wa Tabora.

Akizungumza kwa njia ya mtandao wa Zoom, Askofu Shoo amesema vijana wana mchango mkubwa kwa kanisa na Taifa.

Amesema kama wakijituma kufanya kazi kwa bidii, watatoa mchangao wao kiuchumi kwa kanisa na jamii inayowazunguka.

"Nawaomba msijidharau kwani mnaweza kufanya makubwa kupitia kujituma katika kazi," amesema Askofu Shoo

Katika kongamano hilo, vijana wamechagua neno kutoka Mithali 10:4b lisemalo 'Mkono wake wenye bidii hutajirisha' kuwa ndio taa yao katika maisha.

Mkuu huyo wa kanisa amesema maneno hayo katika mithali ni muhimu sana kwa vijana hivyo kuondokana na dhana ya kupata mali pasipo kufanya kazi.

Katika tamko la vijana hao, lililosomwa na mwenyekiti wao Taifa, Julian Kagambo wameahidi kuepukana na mafundisho potofu ambayo yameshika kasi ya kuwaaminisha watu kupata mali pasipo kufanya kazi.

Wamesema wanaunga mkono na kulipa nguvu neno la Mungu na kuachana na imani potofu za kuamini baadhi ya vitu kupata utajiri huku wakitoa kwa rai kwa Kanisa kuendelea katika kutoa mafundisho.

Aidha, vijana hao kupitia tamko lao, wametoa wito kwa taasisi za kidini na mashirika mbalimbali kutoa elimu ya malezi na makuzi kwa watoto na vijana.

Wamewataka wazazi na walezi kuwa mstari wa mbele katika kuwafundisha vijana na watoto, misingi ya malezi bora kwa vile kupunguza kwa maadili na malezi ni chanzo cha uharibifu wa maadili katika jamii.

Naye Mratibu wa Vijana KKKT nchini, Mchungaji Frank Mng'ong'o amesema katika kongamano hilo, vijana wamefundwa kikamilifu katika kutumia fursa muhimu zinazowazunguka pamoja na kuwaonesha fursa mbalimbali zinazopatikana sehemu mbalimbali nchini na duniani kwa ujumla.

Amesema wamejifunza maadili na ushirikiano miongoni mwao na wengine wenye imani na itikadi tofauti katika maisha.

“Ukweli hawajatoka watupu na kwa vile wametoka sehemu mbalimbali nchini, ujuzi na elimu waliyopata wataenda kuwapa vijana wenzao wanapotoka," amesema

Mshiriki Regina Fredrick amesema kongamano hilo limewabadilisha kimaisha na kutambua ajira ni ngumu na kwamba wanapaswa kutumia fursa mbalimbali zilizopo kufanya kazi na kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Kongamano hilo lilianza Agosti 9, 2022 na kuwakusanya vijana 540 wasichana wakiwa 193 na wavulana wakiwa 347.