Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Shoo: Kwa Mungu hakuna chama

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjiri la Kirutheri Tanzania (KKKT) Dk Fredrick Shoo.

Muktasari:

  • Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo amewataka wananchi kuacha kuingiza siasa katika jambo la kumtumikia Mungu na kuonya wale wanaowanyooshea vidole wanaojitolea kumtumikia Mungu.

Hai. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo amewataka wananchi kuacha kuingiza siasa katika mambo ya kumtumikia Mungu na kuonya wanaowabeza wanaojitolea katika shughuli za Kanisa.

Askofu Shoo ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini wa KKKT, ametoa rai hiyo leo Jumapili Desemba 31,2023 katika usharika wa Nshara, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, wakati akihubiri kwenye ibada iliyoenda sambamba na harambee ya kukamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza ya Kanisa la Betheli.

Katika Harambee hiyo, viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Amir Mkalipa, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika.

Wengine ni Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe, wabunge wa viti maalumu, Halima Mdee na Esther Bulaya pamoja na viongozi wengine wa vyama vya siasa na Serikali na wafanyabiashara.

Dk Shoo amesema baadhi ya watu hawafanyi jambo sahihi kuhusisha masuala ya kisiasa pale wanapojitokeza watu kujitolea kwenye madhabahu ya Mungu.

"Kwa Mungu hakuna masuala ya vyama, katika ibada hii tujitoe,  tena anasema mtoleeni Mungu kwa furaha kwamba ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake, tupo upande wake, sisi kondoo wa malisho yake, tukitambua hilo utaona sababu ya kujitoa, katika kazi ya Mungu.

"Nawasihi sana Mungu akatuguse kwa neno hili, tukamjengee bwana nyumba yake bwana akapate kufurahia na kutukuzwa, tumwombe Mungu na tutii sauti yake na ndipo anaposema tutaona baraka na neema zake,"amesema na kuongeza Dk Shoo.

"Nataka niseme neno moja na nimelisikia mahali, nasema ole wetu pale ambapo kwa roho ileile ya Yuda Iskarioti kuona wivu kwanini mwana wa Mungu apakwe mafuta ya gharama, kwa nini watu wa Mungu wajitoe, kwenye kazi ya Mungu" amesema Dk Shoo

Pia Dk Shoo ameonya wale wanaowaongelea uongo watu wanaojitoa katika masuala ya Mungu na kuwaletea fitna kwa kuwa wanato sana.