Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Athuman Hamis afariki dunia

Muktasari:

Alizidiwa ghafla na kupelekwa MNH kisha kufariki dunia

 

Dar es Salaam. Aliyekuwa mpigapicha mkuu wa magazeti ya Serikali, Athuman Hamis amefariki dunia leo Alhamisi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 4, mjomba wa marehemu, Omary Mchoropa amesema Hamis amefariki usiku wa kuamkia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

“Amefariki asubuhi, usiku alizidiwa na tukamkimbiza hospitali. Tulimfikisha katika kitengo cha dharura na aliwekewa mashine ya kumsaidia kupumua kwa kuwa alikuwa akipumua kwa taabu sana,” amesema;

“Hata hivyo baada ya muda mfupi walikuja madaktari na kutueleza kuwa ndugu yetu amefariki dunia.”

Amesema kwa sasa familia imekutana katika kikao kwa ajili ya kupanga shughuli ya mazishi.

Kufuatia kifo hicho, Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas alitumia ukurasa wake wa Twitter kutoa pole kwa familia ya mpigapicha huyo.

“Kwa niaba ya Serikali tunatoa pole kwa familia na tasnia kwa ujumla. Mola amlaze mahali pema peponi.”