Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aweso ataka mamlaka za maji kutumia mita za luku

Mita mpya za maji za malipo ambazo zinatarajiwa kusambazwa nchi nzima.

Muktasari:

  • Malipo ya kabla ya Maji yataondoa tatizo la wateja kubambikwa ankara kubwa za maji.

Arusha. Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Anthony Sanga kutoa  taarifa kwa mamlaka zote za maji  nchini kuanza kutumia mfumo wa malipo kabla ya matumizi (LUKU) ili wateja walipe maji kutokana na matumizi yao.

Aweso amesema hayo leo Mei 31,2021 mkoani Arusha, wakati  akitembelea  miradi mikubwa ya maji inayosimamiwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (AUWSA)

Amesema endapo mfumo huo utaanza kutumika utasaidia kuweza kupunguza malalamiko kwa wananchi.

“Lazima tuanze na mfumo wa Luku na tutaanzia kwa viongozi na taasisi za serikali ili tutapata uzoefu na kujifunza ndipo twende kwa wananchi,“ aliongeza.

Aweso  amesema wamenunua mitambo katika baadhi ya mamlaka za maji ili kuweza kuona malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa kwa wananchi kama ni kweli na kupunguza ubambikizi wa bili za maji.

Waziri jumaa Aweso akizungumza na maafisa wa idara Maji na serikali Arusha. picha Amina Ngahewa

Sambamba na hilo, pia Aweso amewaagiza mamlaka za maji kote nchi kupitia kwa wasoma mita za maji kuhakikisha wanaposoma mita za maji wanaweza kuwashirikisha wananchi ili waweze kufahamu kiasi cha maji wanachokuwa wametumia .

Kwa upande wake,  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,  Jerry Muro amesema miradi ya maji inayotekelezwa katika wilaya hiyo imekuwa na mafanikio makubwa.

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Arusha,  Justine Rujomba amesema tayari wameshatekeleza miradi mingi ya maji na mpaka kufika Septemba wananchi wote katika Jiji la Arusha watakuwa hawana shida ya maji.