Babu asimulia wajukuu wanne, mkwe walivyofariki Hanang

Hali ilivyo kwenye mji mdogo wa Katesh wilayani Hanang' Mkoani Manyara baada ya kutokea mafuriko.
Muktasari:
- Ni baadhi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya matope yaliyotokea wilayani Hanang’.
Hanang. Maporomoko ya matope yaliyosababishwa na mvua katika mlima Hanan'g mkoani Manyara na kusababisha vifo vya watu 50, yamemwacha kwenye simanzi kubwa mzee Petro Mjenji, aliyepoteza wajukuu wanne na mama yao.
"Nimepoteza wajukuu wanne na mama yao, kijana wangu yeye alisombwa na maji amejeruhiwa kwa sasa yuko anapatiwa matibabu. Ni masikitiko sana,"
"Mimi nakaa upande wa pili wa kijiji, haya mafuriko yalinikuta nikiwa kule juu kwangu, nikasikia kelele kukimbilia huku nikashtuka baada ya kuona hali ilivyo,"amesimulia.
Maporomoko hayo yalisababishwa na mvua iliyoonyesha usiku wa kuamkia jana Jumapili Desemba 3,2023 ambapo sehemu ya Mlima Hanang ilimomonyoka.