Bado vijiji 2,000 umeme kufika Tanzania nzima

Muktasari:

  • Jumla Vijiji 10,127 nchini Tanzania vimeshapatiwa umeme kati ya vijiji 12,318 vilivyopo.

Dodoma. Jumla Vijiji 10,127 nchini Tanzania vimeshapatiwa umeme kati ya vijiji 12,318 vilivyopo.

 Kwa hesabu hiyo, ni vijiji 2,191 kwa Tanzania nzima ndivyo ambavyo havina umeme lakini Serikali imesema kuwa inakwenda kumaliza tatizo hilo.

Takwimu hizo zimetolewa leo Mei 31, 2023 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati akizungumza kwenye wasilisho la hotuba yake kwa bajeti ya mwaka 2023/24.

Makamba amesema kuwa umeme utafika katika vijiji vyote kwenye bajeti aliyoomba ya mwaka huu ikiwemo vitongoji vingi ambavyo wabunge wamepewa nafasi ya kuchagua kitongoji kipi anataka upelekwe.


Waziri amesema kuwa wakati wanaendelea kupeleka umeme katika vijiji mbalimbali, zoezi la kupeleka umeme katika vitongoji nalo linaendelea kama kawaida hivyo wanaendelea kuvipunguza.

“Kila mbunge kwa mwaka huu atachagua umeme uende katika kitongoji gani wakati mpango kabambe wa kumalizia vijiji tuingie kwenye vitongoji ukiendelea,” amesema Makamba.

Mbali na umeme, lakini Waziri ametangaza kuwa mpango wa ugawaji wa majiko vijijini utaendelea ili kuhamasisha matumizi ya gesi kwa Watanzania.