Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balozi Lumbanga: Katiba mpya haiepukiki

Muktasari:

  • Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Marten Lumbanga amesema mabadiliko ya Katiba hayakwepeki, huku akiwataka viongozi wa Serikali na CCM kutopuuza madai hayo.

  

Dar es Salaam. Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Marten Lumbanga amesema mabadiliko ya Katiba hayakwepeki, huku akiwataka viongozi wa Serikali na CCM kutopuuza madai hayo.

Balozi Lumbanga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi na baadaye Rais mstaafu Benjamin Mkapa kabla ya kuwa Balozi nchini Uswisi, aliyasema hayo katika mahojiano na Mwananchi nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam.

“Kwanza niseme its very unfortunate (ni bahati mbaya) kwamba Kikwete aliyeanzisha hili jambo hakuli carry through (hakulifikisha) mpaka mwisho naye kastaafu, ndiyo kwanza linayumba. Laiti angelisukuma lile wakati bado yuko madarakani tungefika tamati tukawa huru.

“Ukweli nji kwamba tunajaribu kucheza na akili za watu. Suala la marekebisho ya Katiba ni suala ambalo haliepukiki. Tukilikwepa tunajaribu kulikwepa kwa muda tu, lakini halitazuilika,” alisema.

Alisema kwa kuwa tayari kuna wananchi na viongozi wenye maoni tofauti, lazima ifike mahali maoni yao yachukuliwe na yafanyiwe kazi.

“Sasa tatizo letu tunasema tu kwamba, aah! Marekani imekuwa huru zaidi ya miaka 200 wamefanya marekebisho ya Katiba mara ngapi? Sasa wenzako walianzia pazuri, wewe ulianzia kule chini unatakiwa uwe na spidi ya haraka kama wenzako? Haiwezekani.

“Tulikuwa na mfumo wa chama kimoja, wenzetu hawakuwa na kitu kama hicho. Mahitaji yanatofautiana sana,” alisema.

Huku akifafanua mabadiliko yaliyotokea kwa miaka 60 ya uhuru wa Tanzania, Balozi Lumbanga alisema, viongozi wa Serikali wanafanya makosa kuwafananisha Watanzania wa sasa na wa miaka 60 iliyopita.

“Jinsi elimu ya wananchi wetu wetu inavyozidi kupanuka, watu wamekuwa na PhD, hata mimi sikuwa na PhD lakini nimekwenda ubalozini nimejiendeleza kule mpaka nimepata. Sasa huwezi ukawachukulia kama watu wa miaka ya 1960.

Pia alisema mabadiliko ya Katiba yanakwamishwa na viongozi wanaotetea masilahi yao binafsi na kutojali masilahi ya wananchi

“Kuna watu wenye ushawishi ukiwagusa hili, wanatetea masilahi yao. Tunazungumzia future (mnustakabali) ya nchi, siyo masilahi yako, tukiyaahirisha haya leo kesho watakuja kuuliza tena,” alisema.

Akirejea mabadiliko ya mfumo wa chama kimoja kwenda vyama viwili, Lumbanga alisema baadhi ya wana CCM walimlaani.

“Huko tunakokwenda huwezi kutegemea kila mtu anaimba wimbo wa CCM, CCM, CCM imara, uimara wa CCM uko wapi?

“Mimi huwa nasema kila siku, Kama siyo Magufuli (hayati Rais John) kuamua kugombea wakati ule, CCM ilikuwa inapoteza. Tulishafanya analysis zetu kabisa tukaona CCM haiendi mbali. Magufuli kuja kugombea ndiyo ime rejuvenate (imeifufua) CCM.

“Leo ukizungumza na viongozi wengine wa CCM ambao wamelala usingizi, mimi huwa nawaambia, ninyi mmebweteka sana, mnadhani leo ni sawa na juzi, lazima mfanye mageuzi ndani ya chama....alieleza.


Alivyogombewa na Mwinyi, Mkapa, Kikwete

Kabla ya kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Lumbanga alishakuwa Katibu Mkuu katika wizara mbalimbali kama Maliasili na Utalii, Wizara ya Ardhi, Viwanda na Biashara na nyinginezo.

Anakumbuka alivyofanya kazi na Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi Wizara ya Maliasili na Utalii kabla na hata alipokuwa Rais alimkumbuka katika kipindi chake cha mwisho na kumteua kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

“Baada ya Mwinyi kustaafu, akaja Mkapa. Nikamwambia, mimi nilikuwa Katibu Mkuu Kiongozi nafasi ya juu kabisa katika uongozi wa Serikali, sasa wewe kama una mtu unamfikiria aje hapa, mlete wala usiwe na wasiwasi, wala siyo kwamba nitakuwa na kinyongo.

“(Mkapa) akaniambia mbona mimi sioni mtu yoyote anayefaa kufanya hii kazi? Yaani wiki mbili tunabishana, akasema mimi nataka wewe unisaidie. Sijisifu lakini ndio ukweli,” alisema.

Alisema hata alipokuja Rais Kikwete alitaka kufanya naye kazi na walivutana karibu mwezi mzima.

“Nikamwambia mimi nimeshakaa hapa miaka 11, mwaka mmoja na nusu na Mzee Mwinyi na miaka 10 yote na Mkapa, unaweza ukafa, majukumu ni mengi.

“Kikwete akaniambia unataka mimi niharibikiwe? Nikamwambia huwezi kuharibikiwa, lakini ni lazima mnionee huruma kukaa mahali pamoja kipindi kimoja kinachosha. Baadaye Kikwete akanielewa,” alisema.

Baada ya kazi hiyo, anasema aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uswisi

“Bila mimi kujua, siku hiyo akamtangaza Luhanjo kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na mimi akaniita na kuniambia nitakupekela kwenye balozi zetu.

“Nilipojua kazi za ubalozi nikajua anataka kunipeleka Msumbiji au Zambia, ningekataa.

“Niende kuuma mbu tena huko? Tulikuwa tunataniana pale, Dar es Salaam naumwa mbu halafu unipeleke tena huko? Basi akanipeleka Geneva.”

Anasema hata huko ilikuwa akae miaka mitatu, lakini aliongezewa hadi ikafika saba, kutokana na sifa alizopewa na maofisa wa Umoja wa Mataifa.