Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barrick Bulyanhulu yatoa fursa kwa wakandarasi wazawa

Muonekano wa Zahanati inayojengwa Kijiji cha Bushing’we Kata ya Bulyanhulu Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga na mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu

Muktasari:

Zahati 18 zimejengwa na kampuni za wazawa katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga ikiwa ni kutambua na kusapoti wakandarasi wazawa.

Shinyanga. Kampuni za ujenzi za wazawa zimeanza kunufaika baada ya mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu kutekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo wa Zahanati inayojengwa Kijiji cha Bushing’we Kata ya Bulyanhulu Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.

Akizungumza na Mwananchi, Mratibu wa Kampuni ya Ujenzi ya Mjasilia, Thomas Mshiru amesema zahanati hiyo ambayo ipo kwenye hatua ya ukamilishwaji, inajengwa kwa Sh88 milioni fedha zilizotolewa na mgodi huo.

“Uwepo wa mgodi mahali hapa umesaidia sana kwani sisi kama wazawa tunapata kazi, tunajifunza mambo mbalimbali ambayo yanafaida katika maisha yetu kwa gharama ya mgodi hivyo kuifanya kampuni yetu ya mjasilia kutoa ajira za muda mfupi kwa watu zaidi ya 100,” amesema Bashiru

Naye msimamizi wa Kampuni hiyo, James Masatu amesema wamepata kazi na kuboresha maisha yao kupitia kampuni hiyo huku akiishukuru kampuni ya Barrick Bulyanhulu kwa kutambua umuhimu wa kutumia wakandarasi wazawa.

Meneja wa Umoja wa vijiji 14 vinavyozunguka mgodi huo, Joseph Lubega amesema wamewatafutia ajira watu zaidi ya 1, 000 wanaotoka kwenye maeneo yanayozunguka mgodi huo ambao wanapata ajira za muda mfupi na wengine za muda mrefu.

“Kampuni zetu za kizawa zinazopata zabuni za ujenzi kupitia Mgodi wa Barrick Bulyanhulu zinapewa watu wa kufanya kazi kwa muda mfupi ili waweze kujipatia kipato na kuendesha maisha lakini pia kuna wengine wa muda mrefu,”amesema Lubega

Kwa upande wake Mrakibu Idara ya Mahusiano kutoka mgodi huo, William Chungu amesema wameamua kutoa fedha hizo kujenga zahanati ambazo hazihusiani na fungu la fedha za huduma kwa jamii (CSR) lengo likiwa ni kujenga mahusiano mazuri kati yao na wananchi wanaozunguka mdodi huo.