Bosi wa TTCL atoa siri ya kutoa gawiwo kwa serikali

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) , Waziri Kindamba 

Muktasari:

Ni baada ya kuhojiwa imewezaje kutoa gawiwo kwa serikali ya Tanzania


Dar es Salaaam. Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema hatua ya kuanzisha mahusiano ya biashara na nchi kadhaa ni moja ya vyanzo vinavyoongeza mapato katika kampuni hiyo na hata kuchagiza kutoa gawio kwa Serikali.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Waziri Kindamba ametoa kauli hiyo leo Julai 26, 2018 wakati wa mahojiano maalumu kupitia kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds TV. 

Msingi wa kauli hiyo unatokana na swali aliloulizwa kwamba TTCL iliwezaje kutoa gawio la Sh1.5 bilioni kwa Serikali inayotokana na mapato ya Sh217bilioni iliyopata Julai mwaka jana.

Kindamba amesema licha ya kujivunia mapato mengi kutoka kwenye mkongo wa taifa pamoja na kituo cha data (data center), shirila hilo limefufua mahusiano na nchi kadhaa ikiwamo MTM ya Zambia, Uganda, Malawi, Congo DR.

“Sasa hivi tuna wateja katika nchi za jirani ambazo hazina bahari, tumefufua mahusiano haya mengi sana, ni biashara kubwa kwa mfano leo hii Rwanda inayosifika kwa ICT katika ukanda wa Afrika Mashariki lakini wanapata huduma kutoka mkongo wa taifa wa mawasiliano Tanzania, kwa hiyo tuna biashara nyingi inayotuletea mapato,” amesema Kindamba.

Soma Zaidi: