BoT: Ukopeshaji bila leseni faini Sh20 milioni

BoT: Ukopeshaji bila leseni faini Sh20 milioni

Muktasari:

  • Kufuatia ongezeko la taasisi, kamouni na watu wanaotoa mikopo katika jamii, Benki kuu ya Tanzania (BoT) imewaonya wananchi juu ya uchukuaji mikopo kwa watu wasiokuwa na leseni

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka wananchi kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au mtu/watu binafsi ambao hawana leseni.

 Hiyo ni baada ya kubaini kuna baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila ya kuwa na leseni, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.

"Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na leseni husika hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha,” imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa leo Alhamisi, Novemba 24, 2022 na Gavana wa BoT.

"Kwa mujibu wa Kifungu cha 16(2)(a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa Sheria hiyo ni pamoja na faini isiyopungua Sh20 milioni au kifungo kwa muda usiopungua miaka miwili.

Kufuatia hilo, BoT imewaasa wananchi kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au mtu binafsi ambao hawana leseni.

"Orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye leseni za biashara ya kukopesha zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ambayo ni www.bot.go.tz,” imeeleza