Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Britam yaunga mkono juhudi za serikali

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam, Farai Dogo, (kushoto), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na Meneja wa Idara ya Bima ya Afya-Britam Insurance Tanzania, George Mwita.

Dar es Salaam. Katika kuunga mkono mkakati Serikali kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma bila kusumbuka, Britam Insurance Tanzania imetambulisha bima zake mpya za matibabu ‘Afya Care’ na ‘Amani Health,’ mahususi kwa ajili ya kutoa huduma ya afya ya kina na unafuu kwa watu binafsi na familia.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Insurance Tanzania, Farai Dogo amesema, “Tunayo furaha kuitambulisha Afya Care na Amani Health, bidhaa ambazo zinaonyesha dhamira yetu ya kutoa huduma bora za bima ya afya kwa wateja wetu.”

“Lengo letu ni kuleta utulivu wa akili kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya, na hivyo kuimarisha ustawi wa wateja wetu."

Amani Health ni bima ya afya mahususi kwa wafanyabiashara, makampuni na vikundi vilivyosajiliwa rasmi ambapo inatosheleza angalau wafanyikazi au vikundi kuanzia vitano pamoja na wategemezi wao.

Kwa upande wake, Meneja wa Idara ya Bima ya Afya-Britam Insurance Tanzania, George Mwita aliongeza, "’Afya Care’ ni bima ya afya ya kipekee kwa ustawi wa mtu binafsi na familia. Kama wewe unatafuta bima thabiti kwa ajili yako binafsi au familia, bidhaa yetu imuendwa kuhakikisha unapokea huduma bora za afya kwa bei nafuu. 

Bima hiyo imeandaliwa kama mkakati mpana zaidi wa kusaidia ukuaji na maendeleo ya wafanyabiashara mbalimbali nchini Tanzania."