Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bwawa la Kufua Umeme Kidatu lafurika maji

Kutoka kushoto ( wenye vikoti vya orange):Kaimu meneja Kituo cha Kufua Umeme Kidatu Mhandisi Manfred Mbyallu, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Steven Kebwe, Mkurugenzi Mkuu Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Lephy Gembe wakiwa katika Ziara ya Kuangalia Bwawa la Kidatu ambalo Maji Yamezidi kiwango cha uwezo wa bwawa hilo: Picha na Saumu Mwalimu

Muktasari:

Mkurugenzi wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema hatua hiyo imetokana na mashauriano baina ya viongozi mbalimbali wa shirika na serikali kutokana na athari zinazoweza kutokea endapo maji hayo hayatafunguliwa

Morogoro. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limelazimika kufungua milango inayozuia maji katika bwawa linalotumika kuhifadhi maji ya Kufua Umeme Kidatu baada ya bwawa hilo kujaa kupita uwezo wake wa kuhifadhi maji.

Mkurugenzi wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema hatua hiyo imetokana na mashauriano baina ya viongozi mbalimbali wa shirika na serikali kutokana na athari zinazoweza kutokea endapo maji hayo hayatafunguliwa

"Maji haya yanaweza tavunja kingo na kutoka kwa presha ambayo itakua ngumu kui'control' na kuleta madhara kwa wakazi waishio pembezoni mwa mto Kilombero na mazao yao lakini kubwa kuharibu miundombinu ya bwawa hili’’ alisema Mramba

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe ambaye alikuwepo katika ziara hiyo ya kuangalia hali ya bwawa hilo pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa aliwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha wananchi wanapewa taarifa ili wachukue tahadhari kuepuka madhara.

Kama bwawa hili likizidiwa na kupasuka jumla ya wakazi 4500 wa vijiji vya Mkamba na Nyange wangeathirika.