CAG aanika matumizi NHIF yazidi michango

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema ukaguzi umebaini kuwa matumizi kutoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya yamekuwa makubwa ikilinganishwa na michango yao.

Katika mwaka 2021/2022 mfuko umepata hasara ya Sh189.65 bilioni ikilinganishwa na Sh93.6 bilioni iliyokuwapo mwaka uliotangulia.

Ameyaeleza hayo wakati akiwasilisha ripoti yake ya ukaguzi ya mwaka 2021/2022 Dar es Salaam Ikulu leo Machi 29, 2022.

"Pia mfuko umekuwa na mtiririko hasi wa fedha katika shughuli zake za uendeshaji, mwenendo huu unaonyesha kuwa michango inaongezeka kwa asilimia 12.9 wakati matumizi yanaongezeka kwa asilimia 24.6 mara mbili," amesema Kichere.

Amesema makadirio ya uwezo wa mfuko kujiendesha kwa Juni 30, 2021 unaonyesha kuwa mapato ya mfuko yataendelea kuwa chini ya matumizi kwa siku zijazo na mfuko utatumia ziada iliyokusanywa jambo ambalo litasababisha ukwasi kuwa hasi ifikapo mwaka 2025.

"Napendekeza kufanyiwa kazi kwa mapendekezo ya ripoti ya wataalamu na kutekeleza yaliyohitajika ili kurekebisha nakisi kama vile kuimarisha usimamizi wa utoaji huduma za afya.