Dar kupata chanzo cha maji cha uhakika

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi nia yake ya kuhakikisha Dar es Salama inapata chanzo cha uhakika cha maji.


Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameweka wazi nia yake ya kuhakikisha Dar es Salama inapata chanzo cha uhakika cha maji.

Ameyasema hayo leo Jumanne Machi 22, 2022 jijini Dar es Salaam katika kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya maji.

Amesema kutokana na ukubwa na umuhimu wa biashara wa jiji hilo ni lazima iwe na chanzo cha uhakika cha maji ndiyo maana ameridhia  kutekelezwa kwa mradi wa maji kutoka bwawa la Kidunda.

“Tunakwenda kujenga bwawa la Kidunda kuhakikisha Dar inapata chanzo cha uhakika wa maji, najua ni gharama na itachukua muda mrefu ila tutajenga, Mungu anajua fedha tutaitoa wapi.

“Pia nimeeelekeza kutafuta namna ya kuchukua maji ya mto Rufiji, najua pia hii ni gharama ila hakuna mbadala wa maji lazima tuwe nayo ya uhakika,”

Rais Samia pia ameipongeza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salama (Dawasa) kwa utendaji wake na kusababisha jiji hilo kupata maji ya kutosha.

“Dawasa imefanya kazi nzuri sana Dar na Pwani na kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa maji katika viwango vya juu.

“Dar upatikanaji wa maji ni asilimia 96, Pwani bado jitihada zinaendelea kuhakikisha mji huo unapata maji ikizingatiwa una viwanda vingi,” amesema.