DC Chuachua: Uchunguzi unaendelea kifo cha padri
Muktasari:
Padri Samson anadaiwa kuuawa Juni 12 kwa kukatwakatwa na mapanga kisha mwili wake kutupwa mto Meta katika mtaa wa Sabasaba jijini Mbeya
Mbeya.Serikali imesema inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha aliyekuwa padri wa kanisa la Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya, Michael Samson ambaye mwili wake aliyeokotwa mtoni siku mbili zilizopita.
Padri Samson wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers) anadaiwa kuuawa Juni 12 tangu alipoondoka kituo cha Vijana kanisa Katoliki Mbeya majira ya saa 12 jioni kabla ya Juni 11 mwili wake kukutwa katika mto Meta maeneo ya Sabasaba jijini hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Rashid Chuachua amesema bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.
"Bado uchunguzi unaendelea kubaini chanzo chake, hakuna aliyekamatwa hadi sasa" amesema Dk Chuachua.
Kwa upande wake Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya, Gervas Nyaisonga amesema hadi sasa hawajaweka ratiba rasmi ya mazishi ya padre huyo kwani leo ndio watakutana na shirika kuweka mipango ya mazishi.
"Ratiba rasmi itatolewa kesho asubuhi kwakuwa leo usiku tutakuwa na kikao na shirika lake hivyo tuwe na subra kila kitu kitajulikana" amesema Nyaisonga.