Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Kessy akagua miradi ya maji yenye thamani zaidi ya Sh2.8 bilioni Iringa

DC Kessy akisomewa taarifa ya mradi wa maji Kijiji cha Makatapola Kata ya Migori

Muktasari:

  • Miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh2.8 bilioni imekaguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Veronica Kessy ikiwa ni katika kutekeleza sera ya kumtua ndoo kichwani mwanamke katika Wilaya yake.

Iringa. Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Veronica Kessy amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya maji katika vijiji vya Makatapola na Mwaleli Kata ya Migori pamoja na vile vya Nyabula na Mlanda katika Kata ya Magulilwa.

Akizungumza na Mwananchi jana Jumanne Juni 27, wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya Miradi ya maji, Kessy amesema kwa ujumla utekelezaji wa miradi hiyo ni mzuri ikiwa baadhi ya vijiji vimeanza kunufaika na huduma hiyo.

Kessy amesema sera ya maji vijijini inamtaka mkazi wa mahali husika kupata huduma hiyo ndani ya mita 400 kutoka katika makazi yake.

“Sera ya maji vijijini inataka Mkazi wa eneo husika kupata huduma ya maji ndani Mita 400 kutoka katika makazi yao,”amesema Kessy.

Akitoa taarifa yake juu ya mradi wa maji  wa Makatapola-Mwaleli, Meneja wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Iringa, Mhandisi Exaud Humbo amesema ujenzi huo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.7 ukiwa na uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya 6,400 wa vijji vitatu.

Aidha, katika mradi wa maji wa Nyabula-Mlanda  Humbo amesema ujenzi huo unagharimu zaidi ya Sh1.1 bilioni huku utekelezaji wake ukiwa ni asilimia 60 mpaka sasa.

Elizei Mlawa ni Mkazi wa Kijiji cha  Mlanda ambaye alitoa eneo lenye ukubwa wa robo tatu  bure kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa mradi huo wa maji katika eneo lake amesema alitoa eneo hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kutatua changamoto ya maji katika eneo lao.

“Baada ya kupewa taarifa za kuletewa mradi wa maji Mimi na familia yangu tulikaa tukaona tutoe eneo letu kiasi cha robo tatu ili kujenga mradi huu wa maji,” amesema Mlawa.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlanda Leonard Julius amekiri kuwa baada ya mradi huo wa maji wa Nyabula-Mlanda kukamilika kila Kitongoji kitanufaika na mradi huo.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makatapola wamesema awali walikuwa wanapata adha ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa kuwa ilikuwa ikiwalazimu kufuata maji ya Bwawa la Mtera huku kwa sasa wakihisi kurahisishiwa maisha yao.

“Nilikuwa nakaa hata siku tatu bila kuoga, ila kwa sasa maisha yamekuwa marahisi," amesema mmoja wa wakazi wa Makotopola, Kata ya Migori wilayani Iringa.

Mpaka kufikia mwezi wa nane kata zote mbili za Migori pamoja na Nyabula jumla ya vijiji 34 vitanufaika na miradi hiyo ya maji mara baada ya kukamilika.