Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Same ataka makandarasi kutumia vibarua wazawa

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni  (wa pili kutoka kushoto) akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo wakati alipokuwa akikagua matengenezo ya barabara ya Same Mashariki.

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewaagiza makandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara wilayani humo kuwatumia vibarua wazawa kwenye kazi zao ili waweze kupata ajira za muda ambazo zitawasaidia kujipatia kipato na kujikwamu kimaisha.

Same. Mkuu wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewaagiza makandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara wilayani humo kuwatumia vibarua wazawa kwenye kazi zao ili waweze kupata ajira za muda ambazo zitawasaidia kujipatia kipato na kujikwamu kimaisha.

Pamoja na kutoa ajira hizo, Mgeni amewataka makandarasi hao kukamilisha miradi kwa wakati na kwa ubora unaoendana na thamani ya fedha ambazo zinatolewa na serikali ili kuepusha migogoro na Serikali.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa maagizo hayo wakati alipotembelea miradi mbalimbali ya matengenezo ya barabara inayotekelezwa katika jimbo la Same Mashariki yenye urefu wa kilomita 47 yenye thamani ya zaidi ya Sh3.8 bilioni.

"Tunaishukuru Serikali kwa kutulete fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika wilaya yetu, mwaka huu wa fedha tumepata Sh3.8 bilioni katika jimbo hili la Same Mashariki kwa matengenezo ya barabara.

"Meneja Tarura wa wilaya hakikisha hawa makandarasi wanapokuja kufanya kazi huku wanato ajira kwa wananchi wa maeneo haya na sio kutokana nao mjini," amesema.

Naye Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango ameishukuru serikali kwa matengenezo ya barabara yenye urefu wa kilomita 47 inayojengwa katika jimbo hilo ambapo amesema itawapunguzia wananchi adha mbalimbali wanazokabiliana nazo kutokana na kutopitika kwa barabara hizo.

"Rais wetu ametufanyia mengi sana na tunamshukuru sana, tunaona tunavyojengea barabara hapa Same kilomita 47, ametukomboa vikubwa,” amesema.

Kwa upande wake, Meneja wa Tarura wilayani humo, James Mnene amesema katika utekelezaji wa miradi ya barabara za Same Mashariki, Serikali imetenga zaidi ya Sh3.8 bilioni kwa ajili ya matengenezo ya barabara katika mwaka wa fedha 2023/24.

"Kwa mwaka huu wa fedha zimetengwa Sh3.8 bilioni na tunaingia mkataba wa matengenezo kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ni asilimia 60 ya bajeti ambayo tumetengewe na miiradi tumeshaitangaza na tayari tumepata wakandarasi na wameanza matengenezo kwa awamu ya kwanza," amesema.

Amesema katika barabara ya Hidaru - Narema yenye kilomita saba serikali imetoa Sh.335 milioni na utekelezaji wake ni wa miezi 6 ambao mpaka Machi mwakani mkandarasi atakuwa ameshakamilisha utekelezaji wa mradi huo.

"Tunaishukuru serikali kwa msaada huu wa barabara, maana kwa miaka mingi tumekuwa tukisafirisha mazao kwa kutumia punda kutokana na kwamba barabara hazipitiki kabisa, unakuta mtu una chakula shambani lakini ikifika wakati wa kuvuna unatumia gharama kubwa za usafiri na hupati faida," amesema