Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Shekimweri afunguka ulevi wa kupitiliza

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, Jabil Shekimweli

Muktasari:

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini (DC), Jabir Shekimweri amesema heshima ya wauza pombe hushushwa na wateja wao ambao huwathaminisha sawa na bei ya pombe hasa wanapokuwa wamekunywa kupitia kiasi.

Dodoma.Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini (DC), Jabir Shekimweri amesema heshima ya wauza pombe hushushwa na wateja wao ambao huwathaminisha sawa na bei ya pombe hasa wanapokuwa wamekunywa kupitia kiasi.

Shekimweri ametoa kauli hiyo wakati akifunga mradi wa Kupunguza Madhara ya Pombe kwa Jamii uliokuwa ukiendeshwa na Tanzania Girls Guard ambao ulikuwa ni kuendesha kampeni za kupinga matumizi ya pombe kwa Kata nne za Jiji la Dodoma.

Amesema matumizi ya pombe kupita kiasi yamewapoteza vijana na kuwaachia umasikini uliotopea huku wengi wakipoteza mwelekeo wao na kushindwa kuchangia katika nguvu kazi ya Taifa.

Amesema wauzaji na wanunuzi wakati mwingine wanaonekana ni watu wa ajabu wote kwa sababu mmoja akinywa kupitiliza lazima atakuwa na akili tofauti na kawaida yake.

“Mwisho wake muuza pombe hujumuishwa na pombe yenyewe kuwa yupo katika kujiuza kama ilivyo biashara yake, lakini yote inatokana na ulevi wa kupita kiasi ambao hauna staha hata kwa jamii,” amesema Shekimweri.

Kiongozi huyo hakutamka kuzuia unywaji wa pombe lakini amesisitiza matumizi kupita kiasi kuwa hayafai na yanawaumiza zaidi vijana na wasichana hivyo akaomba wageukie miradi mingine ya kujiongezea kipato.

Mratibu wa mradi huo, Valentina Gonza amesema katika kata za Makulu, Iyumbu, Kikuyu Kusini na Kikuyu Kaskazini ambako walifanya kazi kwa miaka mitatu, wamebaini namna ambavyo Taifa linapoteza nguvu kazi kwa kupitia ulevi wa kupindukia ambao hupelekea ushawishi kwa mabinti wa kike kupotea.

Valentina amesema katika utafiti wao wamebaini tatizo pia lipo katika Kata ya Kisinga mkoa wa Iringa ambako walikutana na vitendo vya kikatili vilivyopitiliza lakini vyote sababu yake ilikuwa ni ulevi.

Mwakilishi katika kundi la waendesha bodaboda, Ali Mhozya amesema siyo kila jambo linalofanywa kwa kutofikia malengo au kwa uharibifu huwa limefanywa na walevi wa pombe kwani mengine husababishwa na vitu vingine.

Mhozya amesema uzembe pia unaweza kuchangia mtu akafanya mambo ya ajabu au kusababisha ajali na hata kwenye ushawishi wa mabinti licha ya kuwa ulevi unaweza kuwa na sehemu yake pia kwenye mambo hayo.