Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DC Shinyanga aipa kongole Manispaa ukusanyaji mapato

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.

Muktasari:

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imekusanya zaidi ya Sh5 bilioni, sawa na asilimia 108 ya maengo kufikia Aprili 30, 2023 matarajio yakiwa ni kukusanya zaidi ya Sh6 bilioni ifikapo Juni 30, 2023.

Shinyanga. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi amewataka Madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuongeza ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato kuwezesha halmashauri kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akizungumza wakati wa kikoa cha Baraza la Madiwani kilichoketi Mei 4, 2023, Mkuu huyo wa wilaya ameuagiza uongozi wa Manispaa hiyo kuongeza udhibiti wa mianya inayovujisha mapato kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa hazichepushwi, bali zinaingizwa kwenye akaonti za halamashauri.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura amesema hadi kufikia Aprili 30, halmashauri hiyo imefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh5 bilioni ambayo ni mapato ya ndani, sawa na asilimia 108 ya malengo yaliyokusudiwa.

“Kwa kasi hii, ni matumaini yetu kuwa tutafikia makusanyo ya zaidi ya Sh6 bilioni ifikapo Juni 30, 2023,’’ amesema Satura

Kwa mapato hayo, halmashauri inaendele kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Soko Kuu mjini Shinyanga na Soko la mitumba eneo la Ngokolo.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Masumbuko ametaja ushirikiano miongoni mwaviongozi na watumishi, elimu kwa umma na ushirikishaji kuwa miongoni mwa siri ya mafanikio katika makusanyo ya mapato ya ndani huku akiwahimiza wote wanaohusika na makusanyo kuongeza juhudi, weledi na udhibiti wa mapato.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Anord Makombe ameutaka uongozi wa Serikali na Manispaa ya Shinyanga kuendelea kutekeleza na kusimamia mabadiliko chanya kwenye eneo la makusanyo, udhibiti na matumizi ya mapato.

Kutokana na taarifa hiyo, Mkuu wa wilaya ameupongeza uongozi wa halmashauri kwa mafanikio hayo huku akiwataka kuongeza juhudi zaidi.

"Niwasihi viongozi na watumishi wote wa halmashauri kila mmoja aongeze juhudi katika kutimiza wajibu kuongeza makusanyo ya mapato kuwezesha halmashauri kutekeleza miradi ya maendeleo,’’ amesema Samizi.

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, mkuu huyo wa wilaya amewataka wakazi wa Wilaya ya Shinyanga kila mmoja kulinda na kuhifadhi mazingira katika eneo lake kuepuka madhara ya uharibifu wa mazingira.

“Tupande miti na kuhifadhi vyanzo vya maji katika maeneo yetu huku tukiwachukulia hatua stahiki wote wanaobainika kuharibu mazingira na vyanzo vyetu vya maji,’’ amesisitiza mkuu huyo wa wilaya