Diamond amvuta Koffi Olomide Bongo

Saturday November 21 2020
koffipic
By Mwandishi Wetu

Kolabo za kibabe za M-bongofleva Diamond Platnumz bado zinaendelea, sasa kituo kinachofuata ni kati yake na 'baba ya muziki' kutoka DRC Congo, Koffi Olomide.

Iko hivi, usiku wa kuamkia leo, Koffi alitua Bongo katika Uwanja wa Ndege wa Kimatafia wa Julius Nyerere Terminal 3 na alipokelewa na Diamond Platnumz akiwa na timu yake.

Akizungumza na waandishi habari uwanjani hapo Koffi alisema amekuja TZ kwa sababu ana jambo lake na Diamond na alifafanua zaidi kwamba jambo lenyewe linahusu muziki.

“Niko hapa kwa ajili ya kufanya kazi na Daimond. Na ni kazi inayohusiana na kimuziki,” alisema Koffi.

Akizungumzia tukio hilo, Meneja wa msanii Diamond anayefahamika kwa jina la Sallam SK, alidokeza kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba ujio wa Koffi ni kwa ajili ya kutengeneza ngoma na Diamond, aliandika; “Wimbo huu ni HIT tayari.” Maneno hayo yaliambatanishwa na picha inayowaonyesha Diamond, Koffi na Sallam.

Kollabo ya Diamond na Koffi itakuwa ya nne kwa Diamond kufanya na wasanii kutoka  DR Congo.

Advertisement

Tayari mwanamuziki huyo ameshapiga ngoma na Fally Ipupa (Inama), Ya Levis (Penzi), Innos B (Yope Remix) na mkongwe ambaye kwa sasa ni marehemu, Papa Wemba (Chacun Pour Soi).

Advertisement