Dk Hoseah kuanza na utawala wa sheria TLS

Dk Hoseah kuanza na utawala wa sheria TLS

Muktasari:

  • Rais mteule wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Dk Edward Hoseah ameahidi kutumia nafasi yake kuishauri Serikali, mahakama na Bunge kuhusu utawala wa sheria ili wananchi watumikiwe bila kubagua au kupendelewa.

Arusha. Rais mteule wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Dk Edward Hoseah ameahidi kutumia nafasi yake kuishauri Serikali, mahakama na Bunge kuhusu utawala wa sheria ili wananchi watumikiwe bila kubagua au kupendelewa.

Katika uchaguzi huo uliofanyika mkoani Arusha, Dk Hoseah alipata kura 297 na kufuatiwa na Flaviana Charles aliyepata kura 223, Shehzad Wall (192), Albert Msando (69) na rais wa zamani wa chama hicho, Francis Stola akiambulia kura 17.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa uliofanyika jana kwenye jengo la kimataifa la mikutano la AICC, Dk Hoseah alisema TLS itafanya kazi zake kistaarabu na kusimamia msingi yake.

“Ninajua serikali inafanyaje kazi zake, hivyo nitatumia uzoefu wangu kuhakikisha sheria zenye ukinzani na utawala bora zinafanyiwa mabadiliko yatakayohakikisha kila Mtanzania anafurahia nchi yake kwasababu serikali ina wajibu wa kuongoza nchi kwa kuzingatia sheria na haki,” alisema Dk Hoseah.

Alisema kazi kubwa ya taasisi hiyo ni kusimamia utawala wa sheria nchini kwa kuhakikisha mahakama zilizo huru na TLS iliyo huru na kuwa huo ndio utakuwa msimamo na mwelekeo wao kwa kushirikiana na mamlaka zote za serikali.

Alisema utawala wa sheria unamaanisha kuwa kila mtu yupo na mwenye haki katika macho ya sheria na sheria isibague mtu yeyote kwasababu huo ndio msingi wa uhuru na haki katika misingi ya utawala wa sheria.

“Mahakama lazima ziwe huru zinapotoa maamuzi yake na maamuzi yake yazingatie haki, bunge linapotunga sheria zake lazima liangalie haki na utu wa Watanzania, huku serikali inapofanya kazi zake izingatie utu na haki za Watanzania, sisi kama chama cha wanasheria kazi yetu kubwa itakuwa kuishauri serikali,” alisema Dk Hoseah.

Alisema pia watahakikisha wanawatetea wananchi na akiwa kiongozi wa chama hicho hatarudi nyuma kwa kuheshimu kazi kubwa iliyofanywa na watangulizi wenzake, akiwamo anayemaliza muda wake, Dk Rugemeleza Nshala pamoja na baraza la uongozi ambao wamefanya kazi kubwa.

Dk Hoseah aliongeza kuwa wananchi wategemee TLS kuwa wazi, kuwajibika na kuwatetea wananchi bila kujali rangi zao na matabaka yao kwa kuisimamia na kuishauri serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasan itakua sikuvu na kuwa serikali sikivu watafanya nayo kazi vizuri.

“Sisi TLS ni waungwana hatutatumia lugha ya mapambano,lugha yetu ni ya utu ,tutaongea na seriakli utu,ili usikilizwe na mkubwa lazima ujue namna ya kuongea nae,usipojua kuongea na mkubwa hatakusikiliza,nitatumia uzoefu wangu ndani ya serikali na ninajua namna serikali inavyofanya kazi.