Dk Mwigulu: Deni la Taifa ni himilivu

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema Deni la Taifa ni himilivu.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema Deni la Taifa ni himilivu.

Dk Mwigulu amesema hayo leo Jumanne Januari 4, 2021 Ikulu wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19.

#LIVE: Uwasilishwaji taarifa utekelezaji wa matumizi ya fedha za maendeleo na ustawi wa jamii

Amesema kutokana na tathimini iliyofanyika mwezi Novemba mwaka 2021 inaonyesha kuwa deni hilo ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

“Tathimini ya uhimilivu wa deni uliofanyika Novemba kama ulivyoelekeza Rais, unaonyesha deni letu ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu” amesema na kuongeza

“Katika tathimini hiyo viashiria vinaunyesha kwamaba, deni la Serikali kwa uwiano wa Pato la Taifa ni asilimia 31 ambapo ukomo wa kidunia ni asilimia 55” amesema Waziri Mwigulu

Amesema kwa sasa bado nchi ipo kwenye nafasi nzuri kufikia kwenye kikomo cha deni kidunia.